Ripoti zinasema kuwa, baada ya kupita mwaka mmoja tangu kuanza vita vya ndani vya Sudan Aprili 2023 kati ya jeshi la taifa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), wanawake wamekuwa wahanga wakuu ambapo wamedhulumiwa na haki zao za kibinadamu kukikwa kwa kiwango kibwa.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake, Salima Is’haq (chombo cha serikali), anafichua ukiukwaji na unyanyasaji wa kingono waliofanyiwa wanawake nchini Sudan, na kusisitiza kuwa wanawake wanakabiliwa zaidi na ukatili wa kuhamishwa na kulazimishwa kuondoka makwao na wamepoteza usalama, akiba, na ndoto zao.
Is’haq amesisitiza kuwa, unyanyasaji wa kingono unaohusiana na vita vya ndani nchini Sudan ndio uliokuwa uhalifu mkubwa zaidi dhidi ya wanawake katika mwaka uliopita, akielezea kuwa kulikuwa na kesi 157 zilizorekodiwa, lakini tangu kuharibika kwa mtandao wa mawasiliano na huduma za afya, idadi hiyo haijasasishwa, kwani kuporomoka kwa mfumo wa afya katika maeneo yenye migogoro kumekata mawasiliano na habari.
Makumi ya wanawake wa Sudan wamefanywa watumwa wa ngono wa wapiganaji wa Kikosi cha Msaada wa Haraka katika tukio linalojulikana kama tukio la Hoteli ya Daman huko Nyala.
Ripoti zinasema, maeneo ambayo wanawake walikabiliwa zaidi na ukiukwaji wa haki zao ni maeneo yenye migogoro huko Darfur, El Geneina, Nyala, na Khartoum, hasa maeneo ya Bahri na maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Vikosi vya Msaada wa Haraka, RSF