Afrika Kusini: Israel imeshindwa kwa namna ya kuaibisha katika Mahakama ya ICJ

Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini amesema baada ya utawala haramu wa Kizayuni kukamilisha utetezi wake katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kwamba: utawala wa Israel umeshindwa kwa namna ya kuaibisha katika mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Ronald Lamola amesema: Israel imeshindwa “kwa namna ya kuaibisha” kwa ilivyojaribu kupinga mashtaka yaliyowasilishwa na Afrika Kusini kuhusu mauaji ya kimbari inayofanya katika Ukanda wa Gaza.

Lamola amefafanua kwa kusema: “tuna uhakika kwamba tumewasilisha mashtaka ya kuridhisha, yaliyofafanuliwa kwa kina na mawakili wetu kuhusu jinai zilizofanywa, na leo Israel imeshindwa kwa namna ya kuaibisha”.

Waziri wa sheria wa Afrika Kusini ameongezea kwa kusema, mawakili wa nchi hiyo sasa wamebainisha ukweli wa kuridhisha kwa mahakama na “sheria iko upande wetu.”

Afisa huyo wa Afrika Kusini ametoa maelezo hayo baada ya mwakilishi wa Israel kufika katika kikao cha pili cha kesi iliyofunguliwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki na kuwasilisha hoja zake za kupinga mashtaka yaliyowasilishwa na Afrika Kusini.

Kikao cha kwanza cha kusikiliza mashtaka ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kwa mauaji ya halaiki unayoendelea kufanya utawala huo wa Kizayuni huko Gaza kilifanyika siku ya Alkhamisi.

Mawakili wa upande wa mashtaka wanaoiwakilisha Afrika Kusini walisisitiza mbele ya jopo la majaji wa Mahakama ya ICJ kwamba, utawala wa Kizayuni unatekeleza siasa za ubaguzi wa rangi za Apataidi dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Wiki chache zilizopita, Afrika Kusini iliwasilisha ombi katika mahakama hiyo yenye makao yake makuu mjini The Hague, kutaka kuchunguzwa tuhuma dhidi ya Israel za kufanya mauaji ya kimbari katika vita vya Gaza…/

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *