Afungwa jela miezi 13 kwa kuandika sentensi moja ya kuunga mkono Muqawama wa Palestina

Mahakama ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel imemhukumu Mpalestina mmoja anayeishi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu kifungo cha miezi 13 jela kwa kuandika mtandaoni sentensi moja ya kuunga mkono muqawama wa Palestina.

Mahakama za utawala wa Kizayuni zinawakamata na kuwaweka kizuizini Wapalestina kwa sababu tofauti na kwa madai mbalimbali hewa na ya uwongo.
Kwa mujibu wa ripoti ya kanali ya habari ya Kizayuni ya Kan, Mousa Halaf, Mpalestina mwenye umri wa miaka 39 anayeishi Baitul Muqaddas (Jerusalem), amehukumiwa kifungo cha miezi 13 jela kwa kile mahakama ya utawala wa Kizayuni ilichokiita “kuchochea kufanya mauaji na kuunga mkono mashirika ya kigaidi”.
Kulingana na ripoti hiyo, Halaf amehukumiwa kifungo cha miezi 13 jela kwa kuandika ujumbe kwenye akaunti yake ya Facebook.
Ripoti hiyo ya chaneli ya habari ya Kan imeeleza kuwa, kosa la Mpalestina huyo ni kwamba aliandika juu ya picha ya mmoja wa wanamapambano wa muqawama wa Palestina ambao miezi michache iliyopita walitekeleza operesheni ya kujitolea kufa shahidi huko Tel Aviv: “shujaa ametoa maisha yake katika njia ya Quds”
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *