Aghalabu ya nchi za Kiislamu zatangaza Alhamisi kuwa siku ya kwanza ya Ramadhani

Nchi nyingi za Kiislamu katika eneo la Asia Magharibu au Mashariki ya Kati zimetangaza Alhamisi, Machi 23, kuwa mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Kamati ya Istihlal (kuutafuta mwezi mwandamo) ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imetangaza kuwa Alhamisi ya kesho  23 Machi itakuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Jana Idara ya Mahakama ya Saudi Arabia ilitangaza kwamba kwa kuwa mwezi haukuonekana Jumanne jioni, leo Jumatano ndiyo siku ya mwisho ya mwezi wa Shaban na Ramadhani itaanza kesho Alhamisi.

Televisheni ya Al Jazeera imeripoti kuwa, Kamati ya Istihlal  nchini Qatar pia iimebaini kuwa Alhamisi ni siku ya kwanza ya Ramadhani.

Hali kadhalika wahusika nchini Kuwait na Umoja wa Falme za Kiarabu pia wametangaza kwamba mwezi mwandamo haukuonekana Jumanne jioni na, kwa hiyo, Jumatano ndiyo siku ya mwisho ya Shaaban.

Kwa mujibu wa Idara ya Awqaf ya Kisunni ya Iraq pia, Alhamisi itaashiria mwanzo wa mwezi wa mfungo. Hali kadhalikak Ofisi ya Ayatullah Sistani, Marjaa Taqlid wa Mashia Iraq nayo imetangaza katika taarifa kuwa Alhamisi itakuwa siku ya kwanza ya Ramadhani.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limenukuu Baraza la Fiqh la Wizara ya Awqaf ya nchi hiyo ya Kiarabu likitangaza Alhamisi kuwa siku ya kwanza ya Ramadhani.

Lebanon, Sudan na Misri ni miongoni mwa nchi nyingine za Kiislamu katika Mashariki ya Kati ambako Waislamu wataanza kufunga siku ya Alhamisi.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *