Aina mpya ya virusi vya corona ya IHU yagunduliwa Ufaransa, inabadilika zaidi kuliko omicron

Wanasayansi nchini Ufaransa wamegundua spishi mpya ya corona ya B.1.640.2 ambayo imepewa jina la IHU, ambayo wanasema inabadilika kwa kasi zaidi kuliko ile ya omicron iliyogunduliwa nchini Afrika Kusini mwezi Novemba mwaka jana.

Inasemekana kuwa spishi mpya ya IHU huenda asili yake ikawa nchini Cameroon baada ya watu 12 waliopatikana karibu na mji wa Marseilles wakiwa wameambukizwa kirusi hicho kubainika kuwa waliingia Ufaransa wakitokea nchini humo.

Mbali na Ufaransa, spishi hiyo ya corona inayoendelea kuchunguzwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) bado haijaripotiwa kugunduliwa katika nchi nyingine yoyote.

Kwa mujibu wa wanasayansi wa Ufaransa, taarifa kuhusu kirusi hicho ni mfano mwingine wa kuibuka kusikoweza kutabirika kwa spishi mpya za  SARS-CoV-2  katika eneo lolote lile la kijiografia duniani.

Hata hivyo mtaalamu wa maradhi ya kuambukiza Eric Feigl-Ding anasema kuibuka kwa spishi mpya hakumaanishi kuwa virusi hivyo ni hatari zaidi kuliko vya kabla yake.

Hayo yanaripotiwa huku spishi ya omicron inayosambaa kwa kasi ikiwa hadi sasa imshaeenea katika nchi zaidi ya 100 duniani…/

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *