Al Houthi: Maadui wanalenga kuitawala Yemen kupitia kuibua mifarakano

Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen ameonya kuhusu njama za maadui za kuibua fitina na mifarakano kwa lengo la kueneza satwa yao katika nchi hiyo.

Faraan: Amesisitiza kuwa, muungano wa kivita unaoongozwa na Saudia dhidi ya Yemen unaendelea kutekeleza jinai hasa katika mji wa bandarani wa Hudaydah magharibi mwa nchi hiyo. Sayyid Abdul Malik Badruddin al-Houthi ameyasema hayo Jumatatu jioni mjini Sana’a alipokutana na ujumbe wa viogozi wa kabila la Bayda.

Ameongeza kuwa, mikutano na mijumuiko ya watu wa matabaka mbali mbali ni ishara ya maelewano na ushirikiano katika taifa la Yemen. Amesema sasa ni wakati muafaka wa kustawisha udugu, ushirikiano na amani ya kijamii kwa ajili ya kurejesha amani na utulivu katika mkoa wa Bayda.

Kiongozi wa Ansarullah amesema wanataka kustawisha amani na kutatua migogoro. Aidha ameashiria kumbukumbu ya Novemba 30, siku ambayo askari wa utawala wa kikoloni wa Uingereza walitimuliwa Yemen na kusema tukio hilo lilikuwa ukurasa wenye nuru katika historia ya nchi hiyo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *