Kufuatia vifo vya watu 23 na kujeruhiwa kwa makumi ya watu katika maandamano katika nchi hiyo ya Kiafrika ya Kenya, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alizitaka mamlaka za nchi hio kuzuiwa ili kutoa nafasi ya mazungumzo kwa waandamanaji.
Kufuatia kuidhinishwa kwa sheria ya ongezeko la ushuru na bunge la Kenya na majaribio ya waandamanaji kukimbilia chombo hiki cha kutunga sheria, polisi waliwafyatulia risasi ili kutawanya umati wa watu waliokuwa wakiandamana. Takriban watu watano waliuawa, makumi ya wengine kujeruhiwa na sehemu za jengo la bunge kuchomwa moto baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Matthew Miller, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, aliwaambia waandishi wa habari : “Tunaomba kuwekwe vizuizi kwa mamlaka ya uongozi ili kurudisha utaratibu na kutoa nafasi kwa ajili ya mazungumzo na waandamanaji.”
Afisa huyu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani pia alisema: Tumesikitishwa na vifo na majeraha ya watu na tunatoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.
Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Ikulu ya Marekani pia alisema kuwa Marekani inafuatilia kwa karibu hali ya Nairobi.
Maandamano haya nchini Kenya yanakuja baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kuitangaza nchi hiyo kuwa miongoni mwa orodha ya “washirika wakuu wasio wa NATO wa Marekani”.
Jina la “mshirika mkuu asiye wa NATO” limetolewa na Amerika kwa nchi ambazo zina uhusiano wa kimkakati na vikosi vya jeshi la nchi hii, lakini sio wanachama wa makubaliano ya NATO.
Marekani inasema kuwa kuweka nchi katika orodha hii itakuwa na manufaa ya kijeshi na vilevile kiuchumi kwao.
Marekani tayari imejumuisha nchi 17 pamoja na utawala wa Israel katika orodha yake ya washirika wakuu wasio wa NATO, miongoni mwa nchi ya Brazil, Qatar, Ufilipino, New Zealand, Argentina, Taiwan, Pakistan na Tunisia.
Rais wa Kenya William Ruto aliliomba jeshi la nchi hiyo kuingilia kati swala kuzima maandamano dhidi ya serikali na kusema kuwa wanajeshi watatumwa kwa ajili ya ulinzi wa mali na amani ya Wakenya ili kuondoa wasiwasi wa watu kwa ajili ya mali zao. Aliongoza kua Maandamano hayo yaliyokua ya amani yaligeuka kuwa chanzo cha uharibifu na ghasia, na kusema kua wahalifu wote wataadhibiwa.
Wapinzani wa ongezeko la ushuru nchini Kenya, wanaolichukulia kuwa janga la kimaisha, wamemtaka Rais William Ruto kujiuzulu.
Ruto ambaye aliteuliwa kuwa Raisi wa nchi hiyo alishinda karibu miaka miwili iliyopita katika kampeni ya kuunga mkono wafanyakazi maskini wa Kenya, lakini pia anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF kupunguza nakisi ya bajeti kwa ajili ya misaada zaidi na jamii maskini. Inasemekana kuwa lengo la serikali kuwasilisha mswada huu ni kukusanya dola bilioni 2.7 za ushuru wa ziada katika juhudi za kupunguza mzigo mkubwa wa madeni ya nje ya Kenya.
Balozi na ofisi za kidiplomasia za nchi 13 za Magharibi, zikiwemo Canada, Ujerumani, Uingereza na Marekani, zilisema katika taarifa yake ya pamoja, “Tumeshtushwa na matukio ya vurugu tuliyoshuhudia nje ya bunge la Kenya.”