Amir-Abdollahian: Iran inafuatilia kuhakikisha kunafikiwa makubaliano ya kudumu katika mazungumzo ya Vienna

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria mazungumzo ya Vienna ya kuondolewa vikwazo taifa hili na kusema kuwa, Tehran inafuatilia kwa nguvu zote kuhakikisha kunafikiwa makubaliano ya kudumu.

Hussein Amir-Abdollahian, amesema hayo katiika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Moscow akiwa pamoja na mwenyeji wake, Sergey Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni na kusisitiza kwamba, kama Marekanii itaangalia mambo kwa uhalisia wake, basi siyo jambo lililo mbali kufikiwa makubaliano katika mazungumzo ya Vienna.

Kuhusiana na kadhia ya Ukraine, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, katika safari yake hiyo mjini Moscow alikuwa amebeba ujumbe wa mmoja wa viongozi wa Ulaya na ameuwasilisha kwa viongozi wa Rusia.

Amesema kuwa, kuna mitazamo mizuri kuhusiiana na suala la kkusaidia kurejesha amani na utulivu nchini Ukraine na kusitisha vita hivyo.

Kadhalika amesema kuwa, Jamhurii ya Kiislamu ya ran imetangaza na kuweka bayana msimamo wake kuhusiana na vita vya Ukraine na kwamba, inasisitiza udharura wa kutumiwa suhula zote ili kuondokana na hali hiyo.

Kwa upande wake Sergey Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema kuwa, Moscow imeridhishwa kikamilifu na matini ya mwisho ya kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA katika hatua ya hivii sasa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *