Hizam al Asad, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, wananchi wa nchi hiyo hawana njia nyingine isipokuwa kuendeleza mapambano ya ukombozi wa ardhi za nchi yao kutoka kwenye makucha ya wavamizi wanaoongozwa na Saudi Arabia.
Dk al Asad amesema hayo katika mahojiano na televisheni ya al Alam na kusisitiza kuwa, ingawa inavyoonekana kijuujuu ni Saudia na Imarati ndio wanaoongoza uvamizi wa Yemen, lakini wananchi wa taifa hilo wanaelewa kuwa, Marekani na Uingereza ndio hasa wanaoongoza uvamizi huo.
Vile vile amesema, muqawama na mapambano dhidi ya muungano vamizi, ndio muelekeo ulio wazi kabisa kwa taifa la Yemen kwani njia nyingine za upatanishi wa Marekani, Ufaransa, Uingereza na duru kieneo zote zimekwama
Kiongozi huyo mwanadamizi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen pia amesema kuwa, ukombozi wa nchi yake na kulindwa hadhi ya damu za mashahidi na wananchi wa Yemen, hauna njia nyingine isipokuwa ya muqawama hasa kwa kuzingatia kuwa, kuendelea na hali ya hivi sasa ambayo si ya vita na wala si ya suluhu kuna madhara makubwa hususan kwa vile dunia hivi sasa imeshughulishwa zaidi na madhara ya vita vya Ukraine.
Vile vile amesema, Marekani inafanya njama za kutumia mihuri yake ya eneo hili yaani Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) na Saudi Arabia kufanikisha malengo ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuimarisha uwepo wake wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja ndani ya ardhi ya Yemen.