Ansarullah: Uhalifu wa Wazayuni mjini Jenin ni nukta ya aibu kwa kutaka kuhalalisha mahusiano

Ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Ansarullah nchini Yemen imesisitiza kuwa, mauaji ya Wapalestina yaliyotekelezwa  na adui Mzayuni huko mjini Jenin ni chanzo cha aibu kwa tawala ambazo zimegeukia kuhalalisha uhusiano na utawala huo ghasibu, kwa sababu kwa kupiga hatua katika swala la kuhalalisha inampa nguvu adui Mzayuni na kumhimiza kuwakalia kwa mabavu na kuendeleza jinai zake dhidi ya watu wa Palestina.

Kituo cha habari cha harakati ya Ansarullah kilichapisha taarifa kutoka ofisi ya kisiasa ya Ansarallah na kutangaza: Taifa la Palestina liliwasilisha mashahidi 10 na makumi ya majeruhi katika kambi ya Jenin kwa utu na heshima.

Imeelezwa katika kauli hii: Mauaji ya umwagaji damu ya watu wa Palestina katika kambi ya Jenin na adui aliyeghafilika si tu kwamba yanadhoofisha azma ya wananchi wa Palestina, bali pia yanaongeza azma yao ya kukabiliana na hujuma za Wazayuni na kujitolea mhanga kwa ajili ya taifa kubwa la Palestina na kwa ajili ya uhuru wa dunia ulio na thamani na ni chanzo cha fahari, na damu ya mashahidi wa taifa la Palestina na jihadi ya mashujaa wake inadhamini kushindwa kwa maadui.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *