Uchunguzi wa hivi karibuni wa maoni unaonesha kuwa asilimia 70 ya wananchi wa Marekani wana wasiwasi wa kutokea vita vya nyuklia.
Kuendelea vita nchini Ukraine na vikwazo dhidi ya Moscow sambamba na kuendelea nchi za Magharibi kuirundikia silaha Ukraine ni sababu ya wasiwasi huo wa asilimia kubwa ya Wamarekani kuhusu kutokea vita vya atomiki duniani. Hivi karibuni Rais Vladimir Putin wa Russia ametishia kuwa nchi yake itatumia nguvu na suhula zote ilizo nazo kuhakikisha njama za Wamagharibi dhidi ya Moscow hazifanikiwi huko Ukraine.
Kiwango cha Wamarekani wenye wasiwasi wa kutokea vita vya nyuklia kimeongezeka kwa kiasi kikubwa kama hicho ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 1945.
Televisheni ya CNN ya Marekani imetangaza kuwa, matokeo ya uchunguzi wa karibuni wa maoni yanaonesha kwamba karibu asilimia 70 ya Wamaekani wana wasiwasi kwamba mgogoro wa Russia na Ukraine utaishia kwenye vita vya nyuklia.
Ikumbukwe kuwa katika historia nzima ya mwanadamu, ni Marekani pekee ndiyo iliyowahi kutumia silaha za nyuklia dhidi ya maadui zake.
Tangu Marekani ilipofanya mashambulizi hayo ya kikatili na jinai kubwa katika miji ya Hiroshima na Nagazaki nchini Japoan mwezi Agosti 1945, hakuna mwaka wowote uliopita vivi hivi bila ya walimwengu kuwa na wasiwasi wa kutokea vita vya atomiki duniani.
Nchi zenye idadi kubwa zaidi ya vichwa vya nyuklia ulimwenguni hivi sasa ni Marekani na Russia na ni kwa sababu hiyo ndio maana walimwengu wana wasiwasi mkubwa wa kutokea vita vya atomiki kutokana na utesi unaoendelea huko Ukraine.