Askari 13,000 wa Ukraine wameuawa katika vita na Russia

Mykhailo Podoliak, mshauri wa Rais wa Ukraine, amesema: vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo hadi sasa vimepoteza kati ya wanajeshi 10,000 hadi 13,000 katika vita dhidi ya Russia.

Podoliak amesema katika mahojiano na Channel 24 TV ya Ukraine: “tuna takwimu rasmi kutoka kwa makao makuu ya ya Kamandi ya juu zinazoonyesha idadi hii ya wanajeshi waliouawa katika vita.”
Mshauri wa rais wa Ukraine ameongeza kuwa: idadi ya wanajeshi waliojeruhiwa ni kubwa zaidi ya waliouawa.
Kabla ya hapo mnamo mwishoni mwa mwezi Agosti ilitangazwa kuwa idadi ya askari wa Ukraine waliouawa na kujeruhiwa katika vita dhidi ya Russia ni takriban elfu tisa.
Miezi 9 imepita tangu vita vya Ukraine, ambapo licha ya maafa na matokeo yake makubwa na hasi ya kisiasa, kijeshi, kiuchumi, kijamii na hata kiutamaduni, nchi za Magharibi zinaendelea kutuma silaha nchini humo kukoleza zaidi moto wa vita hivyo
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *