Mitandao ya kijamii imesambaza video inayomuonyesha askari mmoja wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel akiwasihi vijana Wapalestina katika eneo la Al-Khalil, Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan wahitimishe muqawama na mapambano dhidi yake yeye na wanajeshi wenzake.
Katika video hiyo ambayo imeangaliwa na watu wengi sana, anaonekana askari wa utawala wa Kizayuni akiwataka vijana Wapalestina wasitishe muqawama na upinzani wao huku akisema: tumechoka taabani, basi tena! nendeni zenu…nendeni zenu…nimechoka!
Mtu aliyerekodi tukio hilo ameiambia televisheni ya Aljazeera ya Qatar: “askari huyu alikuwa akijaribu kuhitimisha mapigano na vijana Wapalestina, lakini mapigano hayo yalikuwa yameendelea kwa muda mrefu, na inavyoonekana jambo hilo ndilo lililomkasirisha yeye na askari wenzake, kwa sababu yalikuwa yamewachosha mno na kuwaacha hoi”.
Katika siku za mwisho wa wiki iliyopita, maeneo mbalimbali ya Al-Khalil kusini mwa Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan yalishuhudia muqawama na mapigano makali yaliyosambaa kila upande kati ya vijana Wapalestina na askari wa utawala haramu wa Kizayuni.
Katika mapigano hayo yaliyopamba moto zaidi katika maingilio ya kambi ya al Fawaz na kijiji cha Kharasa kusini mwa Al-Khalil na katika kambi ya al-Arub, askari wa utawala wa Kizayuni walifyatua risasi za sauti na mabomu ya kutoa machozi kukabiliana na vijana Wapalestina.