jafari

Umoja wa Mataifa wataka kukabidhiwa madaraka kwa amani nchini Bangladesh

Umoja wa Mataifa wataka kukabidhiwa madaraka kwa amani nchini Bangladesh

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza udharura wa kuhamishwa madaraka kwa njia ya amani nchini Bangladesh, akitoa wito wa kuwajibishwa maafisa wa serikali ya nchi hiyo waliohusika na mauaji ya mamia ya watu na kujeruhiwa maelfu ya waandamanaji katika maandamano ya hivi karibuni dhidi ya serikali. Volker Türk amesema kuwa uhamishaji…

Serikali yatoa wito kwa Wakenya nchini Lebanon kuhama

Serikali yatoa wito kwa Wakenya nchini Lebanon kuhama

Nchi kadhaa zimewataka raia wao kuondoka nchini Lebanon, huku hofu ikiongezeka ya mzozo mkubwa katika ukanda wa Mashariki ya Kati. Serikali ya Kenya kupitia Idara ya Mambo ya Nje ya Masuala ya Diaspora, imetoa wito kwa raia wake wanaoishi na kufanya kazi nchini Lebanon kujiandikisha ili kuhamishwa mara moja kutokana na hali ya mvutano inayoongezeka…

Tanzania inataka kuwafurusha Wamasai kwa ajili ya wanyamapori – Wenyeji wapinga Hatua hiyo

Tanzania inataka kuwafurusha Wamasai kwa ajili ya wanyamapori – Wenyeji wapinga Hatua hiyo

Wanajamii wanafanya kampeni kwa wafadhili wa kimataifa kufidia serikali yao na kukomesha ukiukaji wa haki. Dar-es-Salaam, Tanzania – Nadharia ya Joseph Oleshangay ni kwamba maafisa wa serikali katika nchi yake, Tanzania, wanaona watu kutoka jamii yake kuwa chini ya wanadamu. Mwanasheria huyo wa haki za binadamu mwenye umri wa miaka 36 na mwanachama wa kundi…

Mali yakata uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine baada ya shambulio la kigaidi

Mali yakata uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine baada ya shambulio la kigaidi

Mali imetangaza kuwa inakata uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine baada ya Ukraine kukiri kuhusika katika shambulio la kigaidi la hivi karibuni katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Msemaji wa Serikali ya Mpito ya Mali, Kanali Abdoulaye Maiga amesema katika taarifa yake kuwa serikali hiyo imegundua, kwa mshtuko mkubwa, matamshi ya kushangaza yaliyotolewa na  Andriy Yusov, msemaji wa Shirika…

Jeshi la Bangladesh lilitangaza kuunda serikali ya mpito

Jeshi la Bangladesh lilitangaza kuunda serikali ya mpito

Kufuatia kujiuzulu na kukimbia kwa Waziri Mkuu wa Bangladesh, kamanda wa jeshi la nchi hii ya Asia alitangaza kuundwa kwa serikali (mpya) ya muda. Kamanda wa Jeshi la Bangladesh Walker Oz Zaman hii leo (Jumatatu) amethibitisha habari za kujiuzulu na kutoroka kwa Waziri Mkuu Sheikh Hasina na kuwataka raia wa nchi hii “kusimamisha vurugu na…

Shahidi Haniyah  ameidhinisha kuangamizwa kwa Israel: Ustad Syed Jawad Naqvi

Shahidi Haniyah ameidhinisha kuangamizwa kwa Israel: Ustad Syed Jawad Naqvi

Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi (Mkuu wa Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore) Imetolewa katika: Msikiti wa Baitul ul Ateeq Lahore – Pakistan Hotuba ya Ijumaa – 2 Agosti 2024   Hotuba ya Kwanza: Tayyib na Halal vinapaswa kuwa msingi wa maisha yetu ya kiuchumi Hotuba ya Pili: Shahidi Haniyah h ameidhinisha kuangamizwa kwa Israel…

Jeshi la SEPAH latoa taarifa kuhusu kuuawa shahidi Ismail Haniya

Jeshi la SEPAH latoa taarifa kuhusu kuuawa shahidi Ismail Haniya

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) limetoa taarifa nambari tatu inayoeleza na kubainisha jinsi Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS alivyouawa hapa mjini Tehran. Taarifa ya SEPAH inaeleza kuwa, jinai hiyo ya kigaidi iliyopelekea kuuawa shahidi Ismail Haniya ilipangwa na kutekelezwa…

Shambulizi la kigaidi katika mji mkuu wa Somalia lasababisha vifo vya watu 30

Shambulizi la kigaidi katika mji mkuu wa Somalia lasababisha vifo vya watu 30

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, takriban watu 30 waliuawa katika shambulizi la kigaidi usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu wa Somalia. Kwa mujibu wa ripoti ya IRNA ya Ijumaa usiku kutoka Shirika la Habari la Tas, walioshuhudia wameripoti ufyatuaji risasi na milipuko ya guruneti mjini Mogadishu. Pia, vyombo vya habari vya…