Mtoto wa Museveni hajajiuzulu, Jeshi la Uganda lakanusha
Jeshi la Uganda limesema leo Jumatatu kwamba mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye anatajwa kuwa ndiye atakayerithi miikoba ya baba yake kama rais ajaye wa Uganda, hajajiuzulu. Muhoozi Kainerugaba alitangaza kwenye mtandao wa Twitter mnamo Machi 8 kwamba amestaafu kutoka kwenye jeshi baada ya utumishi wa zaidi ya miaka 20….
Zaidi ya wanamgambo 200 wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab wameangamizwa nchini Somalia
Zaidi ya wanamgambo 200 wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab wameangamizwa nchini Somalia kufuatia operesheni ya kijeshi ya jeshi la nchini hiyo. Taarifa ya jeshi la Somalia imethibitisha kutokea mauaji hayo dhidi ya wanachama wa kundi la kigaidi la al-Shabab na kueleza kwamba, operesheni hiyo ya jeshi imetekelezwa katika mji wa Galguduud. Miongoni mwa waliouawa…
Umoja wa Mataifa : Tunahitajia kiasi cha dola milioni 205 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa jimbo la Tigray
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, unahitajia kiasi cha dola milioni 205 kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa jimbo la Tigray. Hayo yameelezwa na Stephane Dujarric, msemaji wa Umoja wa Mataifa katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya umoja huo mjini New York na kueleza kwamba, asasi hiyo inahitajia…
Kutekelezwa oparesheni ya kuvunja mzingiro dhidi ya Yemen ndani ya ardhi ya Saudia
Brigedia Jenerali Yahya Saree, Msemaji wa Jeshi la Yemen mapema wiki hii alitangaza kuhusu kutekelezwa oparesheni ya kuvunja mzingiro dhidi ya Yemen iliyotekelezwa ndani ya ardhi ya Saudia. Kwa upande wa jiografia, oparesheni hiyo ya kuvunja mzingiro imetekelezwa huko Riyadh na pia katika maeneo ya kusini mwa Saudi Arabia yanayopakana na Yemen. Aidha kwa upande…
Shambulizi katika mtandao mkubwa zaidi wa kijasusi wa utawala wa Kizayuni wa Azabajani Magharibi
Mkurugenzi Mkuu wa Ujasusi wa Azabajani Magharibi aliripoti shambulio la askari wasiojulikana wa Imam Zaman (as) kwenye mtandao mkubwa zaidi wa kijasusi wa utawala wa Kizayuni wa jimbo hilo. Mkurugenzi Mkuu wa Ujasusi wa Azabajani Magharibi Jumamosi jioni katika kikao cha zaidi ya saa 4 na waandishi wa habari aliongeza: “Mwaka huu, tuliupiga mtandao mkubwa…
Maandamano makubwa ya kupinga Israel nchini Uturuki
Wananchi wa Uturuki jana Ijumaa, kwa mara nyingine tena walimiminika mabarabarani katika maandamano ya kulaani ziara tata ya rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini mwao. Waturuki walioshiriki maandamano ya jana walikuwa wamebeba bendera za harakati za mapambano za Hizbullah ya Lebanon na Ansarullah ya Yemen, na vilevile picha za Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani,…
Saudi Arabia yawanyonga watu 81 ndani ya siku moja, watu 7 kati ya walionyongwa ni Wayemeni
Kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari, Saudi Arabia iliwanyonga watu 81 katika siku moja kwa uhalifu unaohusiana na “ugaidi”, Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia imethibitisha mkasa huo wa hukumu za kifo za watu 81 na kutangaza kuwa imetekeleza hukumu hiyo kwa watu hao. Shirika la habari la AFP…
Tanzania Kutumia Jeshi la Urusi Kuwaokoa Wanafunzi Waliokwama Ukraine
Wanafunzi hao waliokuwa wanasomea katika Chuo Kikuu cha Sumy nchini Ukraine, watahamishwa hadi eneo salama nchini Urusi ili kuepuka vita.Wanafunzi hao watapokelewa na jeshi la Urusi kwenye mpaka wa taifa hilo. Hatua hiyo ni kufuatia mazungumzo ya kidiplomasia kufanyika kati ya serikali ya Urusi na Tanzania kuridhia. Tanzania imetangaza kuwa Urusi itawasadia wanafunzi Watanzania waliokwama…