jafari

HAMAS yatoa jibu kwa Australia : HAMAS ni harakati ya kitaifa ya ukombozi inayopambana dhidi ya madhalimu kwa mujibu wa sheria za kimataifa

HAMAS yatoa jibu kwa Australia : HAMAS ni harakati ya kitaifa ya ukombozi inayopambana dhidi ya madhalimu kwa mujibu wa sheria za kimataifa

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani vikali hatua ya serikali ya Australia ya kuitambua harakati hiyo ya muqawama inayopigania ukombozi wa Palestina kuwa ni kundi na kigaidi. Taarifa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS  ikmesisitiza kuwa, Israel ndio inayopaswa kutangazwa kuwa utawala wa kigaidi kutokana na jinai zake za kila…

Ali Khamenei : Uongozi wa Muqawama Asia Magharibi wayakata makali majigambo ya ubeberu

Ali Khamenei : Uongozi wa Muqawama Asia Magharibi wayakata makali majigambo ya ubeberu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, muqawama unaokua na kuzidi kupata nguvu katika eneo la Asia Magharibi umesambaratisha kiburi na majigambo ya ubeberu. Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo sambamba na kukaribia kumbukumbu ya harakati ya kihistoria ya wananchi wa Tabriz ya 29 Bahman 1356 Hijria Shamshia (18 Februari 1978) wakati alipozungumza kwa…

Mlipuko uliotikisa Mogadishu / Mji Mkuu wa Somalia

Mlipuko uliotikisa Mogadishu / Mji Mkuu wa Somalia

Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada katika mkutano wa hadhara uliokua katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, huku wanamgambo wa al-Shabaab wakishambulia vituo vya polisi. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, waziri wa usalama wa mambo ya ndani wa Somalia alisema kuwa mnamo Jumatano asubuhi, wanamgambo wa al-Shabaab walishambulia vituo vya polisi na…

Vituo vya polisi Mogadishu vyashambuliwa na Al Shabaab

Vituo vya polisi Mogadishu vyashambuliwa na Al Shabaab

Wanamgambo wa kundi la al Shabaab wa nchini Somalia mapema leo wameshambulia vituo vya polisi na vya upekuzi katika mji mkuu Mogadishu. Kundi hilo la kigaidi limefanya hujuma hiyo huku Somalia ikijiandaa kwa uchaguzi wa rais ulioakhirishwa mara kadhaa. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, watu sita wamepoteza maisha katika mashambulizi ya leo ya al Shabaab…

Muungano vamizi wazidi kushambulia mji mkuu Sana’a na miji mingine

Muungano vamizi wazidi kushambulia mji mkuu Sana’a na miji mingine

Muungano vamizi unaoongozwa na Saudia na Imarati unaendelea kufanya jinai dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa nchi ya Kiarabu ya Yemen. Tangu mwezi Machi 2015 hadi hivi sasa, kila siku wananchi wasio na hatia wa Yemen wanamiminiwa mabomu na makombora na wavamizi wa nchi yao wanaoongozwa na Saudi Arabia na Umoja wa Falme za…

Sheikh Maher Hammoud; Imam Khamenei ni kiongozi wa kihistoria

Sheikh Maher Hammoud; Imam Khamenei ni kiongozi wa kihistoria

Sheikh Maher Hammoud, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanazuoni wa Muqawama amesema katika mahojiano kwamba Imam Khamenei ni kiongozi wa kihistoria. Sheikh Maher Hammoud, katibu mkuu wa Muungano wa Wanazuoni wa Muqawama nchini Lebanon amezungumza na Radio Al-Noor kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran siku ya Alhamisi. Katika mahojiano na ‘Al-Siyasah Al-Youm’ , Sheikh Maher…

Syria yapinga Hatua ya Israel ya kuwafukuza Wapalestina Sheikh Jarrah

Syria yapinga Hatua ya Israel ya kuwafukuza Wapalestina Sheikh Jarrah

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imetoa wito wa kukomeshwa hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel za kuharibu nyumba za Wapalestina na kuwafukuza katika ardhi na makazi yao wakieleza kwamba hatua hiyo ni uhalifu wa kivita. Taarifa hiyo ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imetolewa baada ya walowezi wa Kizayuni kuendeleza…

Bunge la Ethiopia lapiga kura ya kusitishwa mapema hali ya hatari ya miezi sita

Bunge la Ethiopia lapiga kura ya kusitishwa mapema hali ya hatari ya miezi sita

Hatua hiyo ni ishara kwamba mzozo wa umwagaji damu kati ya serikali na vikosi vya waasi wa Tigray unaweza kupungua. Uamuzi wa Bunge la Ethiopia utaanza kutekelezwa hivi karibuni. Ethiopia ilitangaza hali ya hatari mwezi Novemba mwaka jana baada ya vikosi vya wapiganaji wa Tigray kuvamia maeneo zaidi ya Ethiopia na kutishia mji mkuu wa nchi hiyo, Addis…