Maelfu ya Wapalestina washiriki Sala ya Ijumaa Msikiti wa Al Aqsa
Wapalestina wasiopungua 40,000 wameshiriki katika Sala ya Ijumaa wiki hii katika Msikiti wa Al Aqsa ulio katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Palestina la Wafa, Idara ya Wakfu ya Mji wa Quds imetangaza kuwa, idadi ya waumini Wapalestina waliosali Sala ya…
San’aa: UAE isubiri jibu chungu na la kuumiza
Mjumbe wa timu ya mazungumzo ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen amesema Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unapaswa kusubiri jibu chungu na la kuumiza, na kwamba ni jambo la kawaida kujibu vitisho. Abdul Malik al-Ajri amesema: “Utangulizi wa hatua ya Imarati kuingilia masuala ya ndani ya nchini Yemen ulianza pale Wamarekani walipopata yakini…
Wapalestina wautaka Umoja wa Afrika kuiondoa Israel katika umoja huo
Viongozi na makundi ya ukombozi wa Palestina wameutaka Umoja wa Afrika (AU) kufikiria upya uamuzi wa mwaka jana wa kuipa Israel hadhi ya kuwa mwangalizi katika umoja huo. Wito huo wa pamoja umetolewa wakati wakuu wa nchi za Afrika wakikutana mjini Addis Ababa katika mkutano wa kilele wa siku mbili wa jumuiya hiyo yenye wanachama 55,…
jinai za muungano wa Saudia dhidi ya wagonjwa; Watoto 3,000 wa Yemen walio na saratani wanakabiliwa na hatari ya kifo
Jinai za muungano vamizi wa Saudia na Imarati zimewakumba wagonjwa wa Yemen mara hii; Kwa namna fulani, mashambulizi ya muungano huo yamesababisha watoto 3,000 wa Yemeni wenye saratani kua katika hatari ya kupoteza uhai. Katika kuadhimisha Siku ya Saratani Duniani, Dk Taha Al-Mutawakil, Waziri wa Afya katika Serikali ya Wokovu ya Taifa la Yemen alisisitiza…
Saudi Arabia kufanya mageuzi na mabadiliko katika bendera ya taifa, kufuta jina la Allah na la Mtume
Muhammad bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme nchini Saudia ambaye kimsingi ndiye kiongozi wa nchi hiyo ameendelea kufanya mageuzi nchini humo ambapo sasa bendera na wimbo wa taifa kufanyiwa marekebisho. Majlisi Shura ya Saudi Arabia ambayo ndio taasisi ya juu zaidi ya mashauriano ya utawala wa Kifalme imepasisha kwa wingi wa kura muswada wa…
Sayyid Abdul-Malik al-Houthi : Marekani na Israeli ndio maadui halisi wa Waislamu
Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema Marekani na utawala haramu wa Israel ni maadui nambari moja wa Waislamu duniani. Akizungumza Jumanne wakati wa mkutano na wawakilishi wa makabila kutoka maeneo yote ya Yemen, Sayyid Abdul-Malik al-Houthi amesema tawala za Marekani na Israel zinajaribu kutekeleza njama dhidi ya Waislamu kwa kutumia hitilafu zilizopo ndani ya umma…
Ayatullah Khamenei: Ayatullah Golpaygani alikuwa miongoni mwa nembo na nguzo muhimu katika chuo kikuu cha kidini cha Qum
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma ujumbe wa salamu za rambirambi kutokana na kifo cha mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu, Ayatullah Safi Golpaygani aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo. Ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu unaeleza kuwa: Ayatullah Safi Golpaygani alikuwa mmoja kati ya nguzo za chuo kikuu cha Qum (Hauza)…
Ujumbe wa ECOWAS na wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Burkina Faso
Baada ya kupita wiki moja tangu kutokea mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso, ujumbe wa makamanda wa jeshi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) upo katika nchi hiyo na umekutana na kufanya mazungumzo mjini Ouagadougou na wanachama wa Baraza la Utawala wa Kijeshi. Mazungumzo baina ya wanajeshi…