
Umaskini na kuzorota kwa maisha ya Waarabu katika jamii ya Kizayuni
Shirika la Usalama wa Jamii la Israeli lilitoa ripoti mwezi Desemba mwaka jana ya kwamba asilimia Hamsini na Tatu nukta Tatu (53.3%) ya Waarabu wanaoishi katika maeneo yaliyomilikiwa kimabavu wako chini ya mstari wa umaskini. Kwa mujibu wa takwimu hizi, asilimia Ishirini (20%) ya Wayahudi wanaoishi katika maeneo ya Palestina yanayomilkiwa kimabavu na utawala wa Israeli, pia vilevile wako chini ya mstari wa umaskini.