Balozi mwingine wa Israel ajiuzulu kulalamikia serikali ya misimamo ya kufurutu mpaka ya Netanyahu

Baada ya kujiuzulu balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Ufaransa, balozi wa utawala huo nchini Canada naye pia amejiuzulu wadhifa wake kulalamikia baraza la mawaziri lenye misimamo ya kufurutu ada linaloongozwa na Benjamin Netanyahu na kumuunga mkono waziri mkuu wa zamani Yair Lapid ambaye ni kiongozi wa wapinzani wa Netanyahu.

Gazeti la kizayuni la Jerusalem Post limeandika: kama alivyofanya Yael German, balozi wa utawala wa Kizayuni huko Paris, Ronen Hoffman, balozi wa Israel nchini Canada naye pia amewasilisha barua yake ya kujiuzulu akipinga sera ya baraza jipya la mawaziri la utawala huo, na kuwa balozi wa pili wa utawala haramu wa Israel kujiuzulu tangu Netanyahu alipoingia madarakani mwezi uliopita.
Mabalozi hao wawili waliteuliwa na Lapid, waziri mkuu wa zamani na kiongozi wa mrengo unaopinga baraza la mawaziri la Netanyahu.
Hoffman ameandika ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter: “kutokana na mabadiliko ya baraza jipya la mawaziri na kubadilika kwa sera huko Israel, insafu ya binafsi na kitaaluma imenilazimisha kufupisha uteuzi wangu na nitarejea Israel katika msimu huu wa joto.”
Kupitishwa kwa baadhi ya sheria, ikiwemo sheria inayoruhusu wanasiasa wahalifu kuwemo katika baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni, kumechochea maandamano makubwa ya upinzani katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ambazo kwa siku kadhaa sasa zinashuhudia maandamano ya kupinga baraza la mawaziri lililoundwa na Netanyahu.
Hatua za baraza la mawaziri la Netanyahu za kutaka kubadilisha na kurekebisha sheria za mahakama zimeibua sauti za malalamiko za Wazayuni huku Netanyahu mwenyewe akiwa anakabiliwa na kesi tatu za ufisadi na rushwa katika mahakama ya utawala huo.
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *