Balozi wa Tel Aviv mjini Washington: Hatuwaui Raia wa kawaida

Licha ya kwamba raia zaidi ya elfu kumi na moja wameuwawa kishahidi katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Ghaza, balozi wa utawala huo mjini Washington anasema kuwa, mashambulizi ya Israel yanalengwa mno!

Michelle Herzog, balozi wa Tel Aviv mjini Washington, anasema utawala huo unatafuta mpango wa muda mrefu wa Gaza na unashauriana na Marekani kuhusu suala hili.

Katika mahojiano na Fox News, Herzog alisema: Msimamo wetu ni kwamba Wapalestina wanapaswa kusimamia Gaza wenyewe. Jukumu ambalo Mamlaka ya Palestina inapaswa kutekeleza bado haliko wazi na inabakia kuonekana nini kitatokea kwa sababu kila mtu anajua kuwa Mamlaka ya Palestina haiwezi kumsimamia Ramallah sasa.

Balozi wa Israel mjini Washington alidai kuwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina lazima ijirekebishe.

Katika muendelezo wa mahojiano yake pia alisisitiza kuwa Israel haipendezwi na kuikalia kwa mabavu Gaza, bali usalama ni suala linalopewa kipaumbele.

Herzog aliongeza: Hatuko Gaza ili kuikalia. Tuko pale kuharibu vikosi vya Hamas na vitisho dhidi ya Israel na kupunguza uwezo wake wa kushambulia tena na tena. Hili ndilo lengo letu.

Licha ya vifo vya zaidi ya raia 11,000, Herzog alidai kuwa mashambulizi yetu huko Gaza yanalengwa sana.

Watu lazima waelewe kwamba Gaza ni eneo kubwa zaidi la ugaidi duniani, lenye zaidi ya kilomita 500 za vichuguu vya chini ya ardhi. Hatuwaui watu wa kawaida!

Akiendelea na madai yake, alisisitiza: harakati za watu wengi zaidi kuelekea kusini zinatuonyesha kwamba watu hawa hawataki kuwa ngao za kibinadamu kwa Hamas. Tunajua hawatupendi, lakini hawapendi Hamas pia.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *