Ali Bagheri Kani, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa Iran katika mazungumzo ya nyuklia ya JCPOA amesema; kutokana na mazungumzo ya karibuni mjini Vienna, zimepigwa hatua nzuri katika suala la uondoaji vikwazo.
Bw. Kani katika mazungumzo ya Vienna amesema kuwa; katika kipindi cha siku kadhaa za duru ya nane ya mazungumzo, majadiliano yamejikita zaidi juu ya suala la kuondolewa vikwazo.
Baqeri Kani ameongeza kuwa, katika duru hiyo ya mazungumzo kati ya upande wa Iran na upande wa pili majadiliano yameendelea katika nyuga kadhaa; na katika vikao kadhaa yamefanyika mazungumzo na upande wa Ulaya na mratibu wa kamati ya pamoja ya JCPOA kuhusu maudhui ya kupata uthibitisho wa kuondolewa vikwazo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema, katika uga wa uondoaji vikwazo, umefanyika ule unaotajwa kama maandikiano kati ya pande mbili; na hatua nzuri zimepigwa katika siku kadhaa za mwanzoni mwa duru ya nane ya mazungumzo.
Amesema, ana matumaini kuwa baada ya siku kadhaa za kusitishwa mazungumzo kwa sababu ya mapumziko ya mwaka mpya, pande husika zitalishughulikia kwa uzito mkubwa zaidi suala la uondoaji vikwazo.
Duru ya nane ya mazungumzo ya Vienna ilianza Jumatatu iliyopita kwa kikao cha kamati ya pamoja ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA…/