BAKWATA lalaani unyama wa Israel, lawataka Waislamu wote Tanzania kuliombea nusra taifa la Palestina

Huu ulikuwa ni ulikuwa ni moja wapo wa Misimamo ya Bwakwata kuhusu Palestina.

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limelaani vitendo vya kinyama na uadui vinavyofanywa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa taifa madhulumu la Palestina vikiwemo vya kuua raia wasio na hatia.

Kupitia tamko lililosomwa leo Alkhamisi na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Abubakar Zubeir bin Ally, Bakwata limeeleza kuwa vitendo hivyo vinavyofanywa na Israel vinakwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu na vinapingana pia na misingi ya dini kuu duniani, ukiwemo Uislamu.

Tamko hilo la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania limeitaka Jumuiya Kimataifa ichuke hatua zinazohitajika kusitisha udhalimu huo usiokubalika unaofanywa na utawala ghasibu wa Kizayuni.

Katika sehemu nyingine ya tamko hilo la Bakwata, Sheikh Mkuu na Mufti Abubakar Zubeir bin Ally, amewataka Waislamu wote Tanzania, kuitumia Sala ya Ijumaa kusoma dua maalum kuliombea taifa la Palestina na kuendelea na dua za Kunuti katika Sala zote tano kumuomba Mwenyezi Mungu alinusuru Taifa la Palestina na ulimwengu kwa ujumla dhidi ya balaa hilo kubwa la dhulma na unyama wa utawala haramu wa Israel na mabalaa mengine yote ulimwenguni.

Tangu siku ya Jumatatu ya tarehe 10 Mei, jeshi la utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel limeanzisha mashambulio ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa eneo la Ukanda wa Gaza, ambapo hadi sasa Wapalestina wasiopungua 230, wakiwemo watoto 65 wameshauawa shahidi kutokana na mashambulio hayo na wengine zaidi ya 1,500 wamejeruhiwa.

Katika kujibu uchokozi na jinai hizo za kinyama za utawala haramu wa Israel dhidi ya Gaza, makundi ya muqawama ya Palestina yamevurumisha mamia ya makombora kuelekea miji na vitongoji haramu vya utawala ghasibu wa Kizayuni katika ardhi za Palestina unayoikalia kwa mabavu..

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *