Baraza la Usalama la UN litoa wito wa kushirikishwa kikamilifu wanawake nchini Afghanistan

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake juu ya uamuzi wa Taliban wa kuwazuia wanawake kuhudhuria masomo katika vyuo vikuu na kutoa wito wa ushirikishwa kamili na kwa dhati wanawake na wasichana nchini Afghanistan.

Ni baada ya Serikali ya Taliban kusitisha elimu ya chuo kikuu kwa wanafunzi wote wa kike nchini Afghanistan, hatua ambayo imekosolewa na kulaaniwa na jamii ya kimataifa.

Taarifa ya wanachama wote 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imesema kuwa marufuku ya kuhudhuria wanawake na wasichana katika shule za sekondari na vyuo vikuu nchini Afghanistan inaonyesha kupuuzwa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi katika nchi hiyo.

Baraza hilo limeongeza kuwa, kuwapiga marufuku wanawake kufanya kazi katika mashirika ya misaada ya kibinadamu kutakuwa na athari kubwa mbaya na za haraka katika operesheni za misaada ya binadamu nchini Afghanistan, ikiwa ni pamoja na operesheni za Umoja wa Mataifa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisitiza kuwa vikwazo hivyo vinakinzana na ahadi za kundi la Taliban kwa watu wa Afghanistan, pamoja na matarajio ya jamii ya kimataifa na limetaka vifutiliwe mbali.

Volker Turk, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Jumapili iliyopita piia alilaani uamuzi wa Taliban wa kupiga marufuku wanawake kufanya kazi katika mashirika ya binafsi nchini Afghanistan.

Juzi pia Umoja wa Mataifa uliitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kufanya uchunguzi kuhusu jinsi serikali ya Taliban inavyowatendea wanawake wa Afghanistan.

Richard Bennett, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afghanistan amesema kuwa ameiomba Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kuchunguza jinsi kundi la Taliban linavyowatendea na kunyanyaswa wanawake  nchini Afghanistan.

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afghanistan amesisitiza kuwa atafuatilia suala hilo kwa umakini.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *