Baraza la Ushirikiano: Watu wa Palestina hawataridhika na hatua yeyote isipokuwa usitishaji wa vita uvamizi nchini humo

Nchi  zenye uwanachama katika Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi zilitilia mkazo ulazima wa kukomeshwa kwa uvamizi na kukaliwa kwa mabavu kwa nchi ya Palestina na utawala wa Kizayuni na kusisitiza vikali kusitishwa kwa mapigano mjini Ghaza.

Wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi zimesisitiza jioni ya leo (Ijumaa) kuwa matukio ya Ghaza hayatawafanya wananchi wa Palestina waache kudai haki zao.

Huku likieleza kushangazwa na wale wanaozichukulia oparesheni za utawala wa Kizayuni kuwa ni za kujilinda, baraza hili limefafanua: Wananchi wa Palestina hawakubali chaguo lolote zaidi ya kukomesha uvamizi huo.

Kwa mujibu wa Al Jazeera, Baraza la Ushirikiano lilizitaka nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa kupiga kura mara moja kuunga mkono azimio la usitishaji vita Gaza.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi walifanya kikao kisicho cha kawaida tarehe 26 Oktoba mwezi uliopita huko Muscat, mji mkuu wa Oman, ambapo walipitia matukio ya Palestina.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman ilisisitiza katika taarifa yake kwamba katika mkutano huu, ulazima wa kutumwa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza na kuhakikisha usalama wa kutuma misaada hii umesisitizwa.
Washiriki katika mkutano huu wamejadili kuhusu maendeleo ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, ongezeko la ghasia na mashambulizi ya mabomu katika maeneo ya makazi ya Ukanda wa Gaza na utawala wa Kizayuni, jambo ambalo limepelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa maelfu ya watu huko Ghaza.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *