Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kusimamia kazi zake limesisitiza kuwa, Palestina ndio kadhia ya kwanza katika ulimwengu wa Kiislamu kama ilivyo pia suala la Beitul-Muqaddas.
Sisitizo hilo limo katika taarifa ya mwisho ya mkutano wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kusimamia kazi zake.
Taarifa hiyo sambamba na kueleza kwamba, ni hatua ya kuchukiza ya baadhi ya mataifa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel imesisitiza kuwa, hatua yoyote ile ya kufanya mapatano na maadui wa Uislamu na Uislamu ni kinyume kabisa na maslahi na manufaa ya umma wa Kiislamu.
Sehemu nyinginme ya taarifa ya Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi Muadhamu nchini Iran imeeleza kuwa, kuna haja ya kuwa macho sambamba na kuimarisha kambi ya muqawama na mapambano dhidi ya harakati ya kutaka kuwa na ushawishi ya utawala ghasibu wa Israel na kuyaunga mkono mataifa ya Kiislamu kama ya Yemen, Lebanon, Syria na Afghanistan na kwamba, hiyo ni taklifu ya sheria isiyokwepeka.
Mkutano rasmi wa 10 wa duru ya 5 ya Baraza la Wanazuoni Wataalamu linalomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ulianza siku ya Jumanne hapa mjini Tehran na kumalizika Jumatano ya jana.
Aidha wajumbe wa baraza hilo leo wanatarajiwa kukutana na Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.