Barua ya Palestina kwa Baraza la Usalama kuhusu hujuma za walowezi wa Kizayuni

Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikitaka kusitishwa hujuma na mashambulio ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Palestina wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Faraan: Riyadh Mansur, balozi na mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa katika barua zake mbili tofauti kwa Baraza la Usalama na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, hujuma na mashambulio ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina zimeongezeka katika masiku ya hivi karibuni.

Balozi na mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ameutaka Umoja wa Matafa na baraza lake la usalama kuandaa mazingira ya kutekelezwa azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linalotoa himaya ya kimataifa kwa taifa la Palestina.

Walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakkifanya hujuma na mashambulio ya mara kwa mara dhidi ya nyumba za Wapalestina katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Kwa muda mrefu sasa utawala wa Kizayuni umekuwa ukipora ardhi za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwa lengo la kuvuruga muundo wa kijiografia na kijamii katika maeneo ya Wapalestina kwa uungaji mkono wa kila upande wa Marekani.

Utawala wa Kizayuni unaendeleza ujenzi huo haramu wa vitongoji katika ardhi za Palestina huku ukipuuza takwa la jamii ya kimataifa la kusimamisha ujenzi huo kwa kukingiwa kifua na Marekani. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, ujenzi wa vitongoji vyote vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na Israel katika ardhi za Palestina ni kinyume cha sheria.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *