Msemaji wa jeshi la Israel anasema kuwa basi lililokuwa limebeba walowezi katika Ukingo wa Magharibi ndilo lililolengwa katika operesheni ya kuwafyatulia risasi kwa Wapalestina.
Vyombo vya habari vya lugha ya Kiebrania viliripoti kupigwa risasi Wapalestina dhidi ya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan Jumapili asubuhi.
Gazeti la “Yediot Aharonot” liliandika katika habari ya dharura kwamba wapiganaji wa Kipalestina walilipiga risasi basi lililokuwa limebeba walowezi wa Kizayuni katika eneo la “Wadi al-Haramieh”, lililoko kaskazini mwa makazi ya “Ofra”.
Dakika chache baadaye msemaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni alithibitisha habari hiyo na kusema: Dakika chache zilizopita ilipokelewa ripoti kuhusu kupigwa risasi kwa basi la Israel karibu na kijiji cha Selvad katika eneo la Benjamin. Askari wanawasaka washukiwa hao katika eneo hilo.