“BBC” inampango wakuzifunga redio zake za lugha ya Kiajemi na Kiarabu

Idhaa ya Kiingereza ya “BBC” ilitangaza kuwa kutokana na matatizo ya kifedha, itafunga redio zake za lugha ya Kiajemi na Kiarabu huku ikiwaachisha kazi mamia ya wafanyakazi wake.

Wakati ikifichua habari za kufungwa kwa vipindi vyake vya redio kwa lugha za Kiajemi na Kiarabu, idhaa ya Kiingereza ya “BBC” iliripoti kuwa wafanyikazi wake 382 kote ulimwenguni wamepoteza kazi zao katika uamuzi wa kuachishwa kazi.

Kulingana na tovuti ya mtandao wa Al-Mayadeen, Idhaa ya Dunia ya BBC ilitangaza katika taarifa: “Gharama kubwa na ufadhili wa leseni zisizobadilika na za malipo ya pesa zimesababisha uamuzi huu mgumu.”

BBC ya Kiingereza pia ilitangaza kuwa huduma yake ya kimataifa itapunguza kazi mamia ya wafanyikazi kote ulimwenguni wakati idhaa za redio za Kiarabu na Kiajemi zikifungwa.

Idhaa ya Dunia ya BBC iliendelea na taarifa yake na kuongeza: Kulingana na mpango uliopangwa wa kuachishwa kazi na kufungwa kwa vituo vya redio vya BBC Arabic na BBC Farsi, wafanyakazi 382 wamefutwa kazi hadi kufikia sasa.

Kuhusiana na hili, wasimamizi wa mtandao wa BBC wametangaza kuwa inawalazimu kuokoa pauni milioni 28.5 katika idara ya huduma ya kimataifa ya BBC ili huduma hii iendelee kufanya kazi.

Hapo awali, maafisa wa mtandao huu walisema katika taarifa kwamba BBC na mashirika yake ya vyombo vya habari wanapaswa kupunguza gharama zao za kila mwaka kwa pauni milioni 500.

Hii ni pamoja na kuwa katika siku chache zilizopita zilichapishwa ripoti mbalimbali kuhusu utendaji usiokuwa wa kitaalamu wa vyombo hivyo vya habari vya Kiingereza, ikiwemo katika sehemu ya Kiajemi na kukiuka viwango kwa lengo la kuendeleza vurugu nchini Iran.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *