Biashara baina ya Iran, Afrika yapindukia dola milioni 990 ndani ya miezi 7

Miamala ya kibiashara kati ya Jamhuri ya Kiislamu na nchi za Afrika imepindukia dola milioni 990 za Marekani katika kipindi cha miezi saba iliyopita.

Hayo yameripotiwa na gazeti la Financial Tribune ambalo limeeleza kuwa, mabadilishano hayo ya biashara baina ya Iran na Afrika baina ya March 21 na Oktoba 22 ni tani milioni 1.89 zenye thamani ya dola 992.77.

Takwimu za Idara ya Forodha ya Iran zinazoonesha kuwa, katika kipindi hicho cha miezi saba ya kwanza ya mwaka huu wa Kiirani (1401 Hijria Shamsia), Afrika Kusini inaongoza katika orodha hiyo ya miamala ya kibiashara na Iran, kwa tani 462,590 zenye thamani ya dola milioni 254.05.

Aidha nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inaongoza kwa kuwa soko kubwa zaidi la bidhaa za Iran barani Afrika, kwani ilipokea bidhaa za tani 461,840 zenye thamani ya dola milioni 247.62.

Inafuatiwa na Msumbiji iliyopokea bidhaa zenye uzito wa tani 288,305 zilizokuwa na thamani ya dola milioni 160.82 huku Sudan ikipokea tani 221,123 zenye thamani ya dola milioni 122.34.

Hivi karibuni, Ahmad-Reza Alaei Tabatabaei, Naibu mkuu wa Shirika la Kukuza Biashara la Iran (TPO) aliashiria ongezeko la asilimia 45 la mauzo ya bidhaa za Iran barani Afrika na kusema: “Kwa sasa, Ghana ni kituo cha kwanza cha mauzo ya Iran barani Afrika, ikifuatiwa na Afrika Kusini na Nigeria katika nafasi za pili na tatu.”

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *