Hakuna sababu ya kimantiki kwa Marekani kuiunga mkono Israeli. Kutotambulika kwa nchi ya Israeli katika eneo la Mashariki ya Kati inatosha kua ni sababu kwa serikali ya Marekani kupata ufahamu na kutafakari upya uhusiano wake na utawala wa Israeli.
Faraan: “Kwa Hakika utawala wa Israeli hauwezi kudumu kwa muda bila kuungwa mkono na Marekani,” alisema balozi wa utawala wa Bush nchini Saudi Arabia, Bw. Shasfreiman. Kwa sababu kwanza kabisa asilimia 20 hadi 25 ya bajeti ya ulinzi wa utawala wa Kizayuni inatolewa na Marekani, yaani hiyo ni asilimia 26 ya jumla ya bilioni tatu ambazo utawala wa Kizayuni unatumia kila mwaka kwa ajili ya utengenezaji wa silaha za kivita na gharama nyenginezo.
Jingine ni kuwa, kutokana na uungaji mkono na mazingatio ya Kongresi ya Marekani, nusu ya gharama za miradi ya ulinzi na maendeleo ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni hutolewa na Marekani pasi na shaka yoyote. Vilevile Marekani inasimamia gharama nyingi za kuendesha makampuni na kupata mishahara ya wafanyakazi wa Israeli.
Inakadiriwa kuwa, serikali ya Marekani imetumia zaidi ya dola trilioni 1.4 tangu mwaka 1949 katika kuuunga mkono utawala wa Kizayuni.
Hakuna sababu yoyote ya kimantiki kwa Marekani kuiunga mkono Israeli. Kutotambulika kwa nchi ya Israeli katika eneo la Mashariki ya Kati inatosha kua ni sababu kwa serikali ya Marekani kupata ufahamu na kutafakari upya uhusiano wake na utawala wa Israeli.