Bilioni 25 za Uviko-19 zapelekwa kukamalisha ujenzi Veta

Dodoma. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema kati ya Sh64.9 bilioni ilizopewa wizara hiyo kutoka fedha za Uviko-19, Sh20 bilioni zilitengwa kwa ajili ya umaliziaji wa vyuo 25 vya ufundi vinavyojengwa katika wilaya mbalimbali nchini.

Kipanga ameyasema hayo leo Jumapili Julai 3, 2022 wakati Kamati ya Bunge ya Bajeti ilipotembelea ujenzi wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (VETA) wilayani Bahi mkoani Dodoma.

“Lakini Sh8.7 bilioni zilikuwa ni kwa ajili ya furniture (samani) ndio hizi unaanza kuziona sasa. Lakini Sh20 bilioni tulipeleka kwa ajili ya kuanza vyuo vya mikoa katika mikoa minne,”amesema.

Kipanga amesema miongoni mwa vyuo ambavyo vilipelekewa fedha hizo ni Chuo cha Bahi ambapo amesema bado kuna changamoto ya umaliziaji wa chuo hicho.

Amesema fedha zilizopelekwa katika chuo hicho zilikuwa Sh695 milioni ambazo hazitaweza kumaliza kazi za nje katika mradi huo na miundombinu ya umeme, maji pamoja na barabara za ndani ya chuo.

Naye Mbunge wa Ole, Juma Hamad Omary ameshauri ujenzi wa majengo mengine ya vyuo ikiwemo madarasa kuwekwa tarazo badala ya tiles ili kuyawezesha kudumu kwa muda mrefu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *