Binti ya Saddam alitorokaje kutoka nchini Iraqi?

Raghad Saddam, bintiye dikteta wa zamani wa Iraq, alihukumiwa kifungo cha miaka 7 jela kwenye mahakama ya nchi hii. Lakini amekuwa akiishi Jordan kwa miaka mingi.

Raghad Saddam, binti wa dikteta wa Iraq, ambaye amekuwa akiishi Jordan kwa miaka mingi, mara kwa mara ameakisi fikra za kupinga ubinadamu za chama cha Baath na kutamka maneno ya chuki mithili ya babake Saddam Hussein.

Katika mahojiano na idhaa za habari ikiwemo al-Arabiya, ametetea vitendo vya baba yake na bila ya kuzungumzia mauaji ya watu wa Iraq na nchi za kieneo yaliyofanywa na chama cha Baath, ameeleza kua yeye anakichukulia chama hicho kilichovunjwa cha Iraq kuwa ndio njia pekee ya kurudisha amani kwa wananchi wa Iraq.

Mahakama ya Iraq ilimhukumu kifungo cha miaka 7 jela siku ya Jumapili (Oktoba 30) kwa sababu hiyo.Katika hukumu hii iliyotolewa na Mahakama ya Jinai ya Al-Karkh mjini Baghdad, imeelezwa kuwa Raghad Saddam, kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha Sheria inayokataza Shughuli za Chama cha Baath na Vyama vya Kigaidi na Kitakfiri. iliyoidhinishwa mwaka wa 2016) amehukumiwa kifungo cha miaka 7 jela.

Raghad alichapisha video ya Saddam akizungumzia Palestina katika akaunti yake ya kibinafsi kwenye mtandao wa kijamii wa X (zamani wa Twitter) akijibu hukumu hii, lakini hakutaja hukumu ya mahakama ya Iraq dhidi yake.

Lakini ni vipi Raghad Saddam alitoroka kutoka Iraq baada ya kuanguka kwa utawala wa Baath?!

Raghad Saddam alizaliwa mwaka 1967, na mwaka 1995, mume wake, ambaye alikuwa mmoja wa maafisa wa ngazi za juu wa shirika la kijasusi la Saddam, alikimbilia Jordan na kurejea Iraq akiwa na dhamana mwaka 1996, lakini aliuawa na Saddam.

Wakati majeshi ya Marekani yalipoivamia Iraq mwaka 2003, Raghad, ambaye aliona familia yake ikiwa imesambaratika, aliomba hifadhi kutoka kwa serikali ya Jordan, na Amman alikubali ombi la binti wa dikteta aliyekufa wa Iraq.

Katika mwaka huohuo, alikimbilia Jordan kupitia Syria pamoja na dada yake Rena ili kupanga utetezi wa kisheria wa Saddam kutoka eneo la nchi jirani kwa kuajiri wanasheria wenye uzoefu!

Wakati huo huo, serikali ya Iraq imerudia kuomba Interpol kumrudisha bintiye dikteta huyo wa zamani kutoka nchi hiyo jirani.

Raghad anashutumiwa kwa kusaidia kifedha na kuandaa vikundi vya kigaidi vilivyojihami vya Iraq, na kwa sababu hii, Interpol ilitoa hati ya kukamatwa kwake mwaka 2009, lakini kukamatwa kwake kulisitishwa kwa muda na uingiliaji kati na upatanishi wa mamlaka ya Jordan.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *