Mshauri huyo wa zamani wa masuala ya usalama wa Marekani aliionya serikali ya Marekani kwamba kwa sasa mazingatio yetu yapo katika kuimarika kwa uhusiano kati ya Iran, China na Urusi.
John Bolton, mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Marekani, aliionya serikali ya Marekani kwamba anatazama tu kupanuka kwa uwezo wa China duniani na ukaribu wake kwa nchi ya Urusi na Iran.
“Tumeketi kimya katika mda ambao Wachina, Warusi, Wairani na Wakora Kaskazini wanapiga hatua katika kuimarisha uhusiano wao na kuwa tishio katika maeneo tofauti,” Bolton alisema katika kipindi cha redio siku ya Jumapili, kulingana na tovuti ya Hill.
Onyo la Bolton lilikuja baada ya Iran na Saudi Arabia kutangaza siku ya Ijumaa kwamba watarekebisha uhusiano na kufungua tena balozi zao katika mafanikio ya kidiplomasia yaliyoratibiwa na China.
Aliongeza: “Wachina wana mikakati ambayo wanaifuata, lakini sisi tunaruka mara kwa mara kutoka kwenye tawi moja hadi lingine.”
“Mmoja wa washindi wakubwa katika vita kati ya Urusi na Ukraine ni Uchina,” Bolton aliendelea kwa kusema Ikiwa Urusi itashinda, itakuwa ni ushindi kwa mshirika wake ambaye ni China, jambo ambalo pia litaiimarisha.”
Kwa mujibu wa habari, hivi karibuni aliukosoa muungano wa NATO unaoongozwa na Marekani na kusema: “Muungano wa NATO umeshindwa zaidi kuliko baadhi ya viongozi wake wa kisiasa wanavyosema, na huenda Rais wa Urusi Vladimir Putin anaichukulia Ujerumani kuwa sehemu dhaifu ya muungano huo. ” .
Mshauri wa usalama wa taifa wa utawala wa zamani wa Marekani aliongeza kuwa ni vibaya kwa Ukraine na Magharibi ikiwa Kiev haina uwezo wa kujibu mashambulizi ya muda mrefu na ya karibu ya Urusi.