Borrell: Lengo la mazungumzo ya Doha ni kuhuisha utekelezaji wa mapatano ya JCPOA

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya (EU) ameandika katika ujumbe wake wa twiter kwamba lengo la mazungumzo ya Doha ni kuanza kufanya kazi mapatano ya JCPOA.

Baada ya mazungumzo ya Vienna kusita kwa miezi kadhaa; mazungumzo hayo kwa mara nyingine tena yalianza jana Jumanne huko Doha mji mkuu wa Qatar kwa kuhudhuriwa na wawakilishi wa Umoja wa Ulaya, Iran na Marekani. Katika fremu hiyo, Ali Bagheri-Kani Mkuu wa Timu ya Mazungumzo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Enrique Mora Naibu Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ambaye pia ni Mratibu wa Mazungumzo ya Kuondoa Vikwazo walikutana kwanza kabla ya kuanza mazungumzo hayo huko Doha.

Ndio maana Ali Bagheri jana Jumanne aliwasili Doha kwa minajili hiyo. Mazungumzo ya kuondoa vikwazo yamepangwa kufanyika kati ya Iran na Marekani kwa njia isiyo ya moja kwa moja; chini ya uongozi wa mratibu wa mazungumzo ya Vienna Enrique Mora. Kama ilivyotangaza Iran kabla ya kuanza mazungumzo haya, mazungumzo ya Doha ni muendelezo wa mazungumzo yaliyosalia ya Vienna.

Shirika la habari la Farsi limeripoti kuwa, Josep Borrell Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya jana usiku alizungumzia kuanza mazungumzo hayo ya Doha na kusema, lengo la mazungumzo hayo ni kufanikisha kazi ili kurejea katika utekelezaji kikamilifu wa mapatano ya JCPOA.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *