Cairo yaitahadharisha Tel Aviv kuhusu hali ya mambo katika Ukingo wa Magharibi

Cairo imeitahadharisha Tev Aviv kuhusu kushtadi mashambulizi ya utawala huo katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na uwezekano wa kushindwa kudhibiti hali hiyo.

Maafisa husika wa Misri wamekosoa hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuendeleza mashambulizi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kutahadharisha juu ya uwezekano wa kuongezeka mivutano katika eneo hilo. Cairo aidha imetahadharisha kuwa, kama hali ya sasa itaendelea huko Ukingo wa Magharibi, Israel itakumbwa na kipindi sawa na kile ilichokabliliana nacho yaani cha milipuko na ghasia za kisiasa baada ya Abu Mazin, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, kujiuzulu.

Baada ya Cairo kutoa indhari hiyo gazeti la Kizayuni la Haaretz pia limeandika kwamba: Israel inafanya mkakati wa kuzidhibiti idara za usalama za Palestina kwa madai ya kuzuia kuongezeka hali ya mvutano katika Ukingo wa Magharibi ili kutekeleza oparesheni zake za kuwatia nguvuni wanaharakati na Wapalestina wenye silaha katika eneo hilo hususan katika miji ya Jenin na Nablus.

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni jana asubuhi walivamia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwatia nguvuni Wapalestina 22 akiwemo mwandishi habari mmoja na wengine kadhaa waliokuwa wameachiwa huru na utawala huo haramu.

Maeneo makuu ya kamatakamata ya kiholela inayofanywa na utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina ni miji ya al Khalil, Bait Laham, Nablus, Jenin, Ramallah na Quds inayokaliwa kwa mabavu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *