Chuo kikuu cha Daystar Kenya chafuta mkataba na ‘Israel’ baada ya malalamiko ya umma
Siku mbili tu baada ya Chuo Kikuu cha Daystar cha Kenya kutia saini mkataba na ubalozi wa utawala Israel jijini Nairobi kuanzisha ‘Msitu wa Zion’ kwenye chuo chake, taasisi hiyo imebatilisha uamuzi wake kufuatia hasira za wananchi katika mitandao ya kijamii hasa X. Makubaliano hayo, yaliyotangazwa Jumatatu, yalilenga kupanda miti 5,000 ‘ya kibiblia’ kwenye uwanja…
Chad yawataka wanajeshi wa Ufaransa kuondoka nchini humo ifikapo 31 Januauri 2025
Serikali ya Chad imeitaka Ufaransa kuwa imewaondoa wanajeshi wake katika ardhi yake ifikapo Januari 31. Imethibitishwa kwamba takwa hili liliwasilishwa huko Paris jana Disemba 19. Hata hivyo, afisa wa ngazi ya juu wa kijeshi wa Ufaransa, ameviambia vyombo vya habari, kwamba itakuwa vigumu kuondoa kikosi kizima cha jeshi katika kipindi cha wiki saba. N’Djamena inasema…
Mahakama ya Katiba: Rais wa zamani wa Zambia azuiwa kugombea tena urais
Edgar Lungu aliyewahi kuwa Rais wa Zambia amezuiwa kugombea tena kiti cha urais nchini humo na kuzua wasiwasi miongoni mwa wafuasi wake. Mahakama ya Katiba ya Zambia kwa kauli moja imetoa maamuzi kuwa rais wa zamani Edgar Lungu hawezi kugombea kwenye uchaguzi wa 2026 kwa kuwa tayari amehudumu mihula miwili. Mahakama hiyo imeamua kuwa, muda…
Nigeria yaripoti vifo 15,000 vinavyohusiana na UKIMWI kila mwaka
Nigeria inarekodi takriban vifo 15,000 vinavyohusiana na Ugonjwa wa Ukimwi kila mwaka licha ya juhudi za serikali za kukabiliana na kuenea ugonjwa huo hatari katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika. Temitope Ilori, mkuu wa Shirika la Taifa la Kudhibiti Ukimwi nchini Nigeria (NACA) amewaambia waandishi wa habari wakati wa shughuli ya uhamasishaji…
Kwa mara nyingine Ronald Lamola ataka kukomeshwa vita mara moja Ghaza
Kwa mara nyingine tena, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ametaka kukomeshwa vita mara moja katika Ukanda wa Ghaza huko Palestina na kufikishiwa misaada wakazi wa eneo hilo haraka iwezekanavyo. Ronald Lamola alitoa mwito huo jana mjini Cairo Misri baada ya mazungumzo yake na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Badr…
Ghorofa laporomoka Kariakoo Dar e Salaam, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha
Watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha baada ya jengo la ghorofa lililoko Kariakoo jijini Dar es Salaam Tanzania kuporomoka. Taarifa zaidi zinasema kuwa, jengo moja la biashara limeporomoka asubuhi ya leo katika mtaa wa Kongo, Kariakoo Jijini Dar es Saalam na kwamba, juhudi za uoakoji zinaendelea. Kwa mujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walipokea taarifa…
MSF yaanza upya kutoa huduma kwa wananchi waliokumbwa na njaa magharibi mwa Sudan
Shirika lisilo la kiserikali la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limetangaza kuwa, limeanza tena kutoa huduma katika kambi ya wakimbizi ya mji wa El Fasher wa Darfur Kaskazini huko magharibi mwa Sudan kutokana na watu katika kambi hiyo kukumbwa na njaa kali na magonjwa ya kuambukiza. Kundi hilo limesema hayo katika mtandao wa kijamii wa…
Balozi wa Sudan: Israel na vikundi vyake vya wakala vinamchango katika vita nchini Sudan
Balozi wa Sudan mjini Tehran amesema kuwa, kinachoendelea Sudan ni jinai kubwa na kusema kuwa, Israel na makundi ya wawakilishi wake katika eneo hilo ndio wanaoendesha mizozo ya hivi sasa nchini Sudan. Abdul Aziz Hasan Saleh Taha, balozi wa Sudan mjini Tehran, alielezea matukio ya hivi punde nchini Sudan katika mkutano na waandishi wa habari…