Afrika Mashariki

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuacha kutumia sarafu ya dola

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuacha kutumia sarafu ya dola

Benki Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetoa agizo la kupunguza matumizi ya dola ya Marekani katika miamala ya sasa ya bidhaa na huduma mbalimbali nchini humo. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inajaribu kupunguza utegemezi wa uchumi wa nchi hiyo kwa sarafu ya dola ya Marekani, na kuhusiana na hilo, hivi karibuni benki kuu…

Viongozi wa Kiislamu Tanzania walaani vitendo vya ushoga

Viongozi wa Kiislamu Tanzania walaani vitendo vya ushoga

Viongozi wa dini ya Kiislamu nchini Tanzania wameendelea kukemea vitendo vya ushoga vinavyooenekana kushamiri katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Sheikh Alhad Mussa ambaye ni Mwenyekiti wa Maridhiano na Amani Tanzania, ameitaka serikali kuchunguza sakata la ushoga linalodaiwa kufanyika katika Hoteli ya Ramada jijini Dar es Salaam. Alhad ametoa mwito huo katika mkutano wa Semina ya Viongozi…

Mkopo wa Dola Bilioni 2.5 Kutoka Korea Kusini: Je, Tanzania Imeweka Rehani Bahari na Madini Yake?

Mkopo wa Dola Bilioni 2.5 Kutoka Korea Kusini: Je, Tanzania Imeweka Rehani Bahari na Madini Yake?

Dar es Salaam. Madai kwamba Tanzania inaweza kuwa imeweka rehani rasilimali zake za bahari na madini ili kukidhi vigezo vya kupata mkopo wa Dola za Kimarekani bilioni 2.5 kutoka Serikali ya Korea Kusini yanaonekana kutokuwa ya kweli, uchambuzi wa utoaji wa aina hiyo ya mikopo uliofanywa na The Chanzo unaonesha. Madai hayo ni sehemu ya mjadala mkubwa…

Afrika ni eneo la pili kwa ustawi wa kasi kiuchumi duniani, Afrika Mashariki yaongoza

Afrika ni eneo la pili kwa ustawi wa kasi kiuchumi duniani, Afrika Mashariki yaongoza

Jumla ya nchi 41 za Afrika (yaani, 72% ya bara zima) zinatarajiwa kuonyesha viwango vya juu vya ukuaji wa kiuchumi mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana. Hayo ni kulingana na Mtazamo wa Kiuchumi wa Afrika wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Zaidi ya hayo, mwaka wa 2024 na 2025, bara Afrika litadumisha nafasi yake kama…

Mexico yapata Rais wa kwanza mwanamke; ni Sheinbaum

Mexico yapata Rais wa kwanza mwanamke; ni Sheinbaum

Claudia Sheinbaum amechaguliwa kuwa rais wa kwanza mwanamke nchiini Mexico katika ushindi wa kihistoria. Mamlaka rasmi ya uchaguzi ya Mexico imesema kuwa, matokeo ya awali yameonyesha kuwa Sheinbaum meya wa zamani wa Mexico City mwenye umri wa miaka 61 ameshinda kati ya 58% na 60% ya kura katika uchaguzi wa jana Jumapili. Matokeo hayo yanampa…

Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya washirika wa Wagner katika Afrika ya Kati

Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya washirika wa Wagner katika Afrika ya Kati

Wizara ya Fedha ya Marekani ilitangaza Alhamisi kwamba imeziweka kampuni mbili za Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye orodha yake ya vikwazo. kampuni hizo zimekua na uhusiano na Kundi la Russia la Wagner. Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Hazina ya Marekani, makampuni haya mawili yenye majina ya Saarlo Mining Industries na Saarlo Economic…

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lazima jaribio la waasi wa M23

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lazima jaribio la waasi wa M23

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limetangaza kuwa, limezima jaribio jengine la waasi wa M23 la kuutwaa mji wa Sake ulioko Kivu Kaskazini, wakati mapigano yakiripotiwa kwenye miji mingine ya Rutshuru na Lubero. Taarifa zaidi zinasema kuwa, mizinga na aina nyingine za kombora zilitumiwa na pande zote mbili, huku jeshi la serikali likivurumisha mabomu…

Marekani, Umoja wa Ulaya Waichagua Kenya Kujiunga Katika Mapambano Dhidi ya wa Houthi

Marekani, Umoja wa Ulaya Waichagua Kenya Kujiunga Katika Mapambano Dhidi ya wa Houthi

Marekani na Umoja wa Ulaya zaichagua Kenya kujiunga na Ushelisheli katika kukabiliana na washukiwa wa baharini kando ya Bahari ya Hindi. Hii ni baada ya nchi kadhaa kuzua taharuki kutokana na vitisho vinavyotolewa na kundi la wa Houthi kutoka nchini Yemen na wengine kutoka Somalia. Kulingana na Jeshi la Wanamaji la Umoja wa Ulaya, Kenya…