Kufanyika kwa Mkutano wa Quds, turathi za pamoja katika dini za mbinguni na mhimili wa umoja kati ya Umma wa Kiislamu nchini Tanzania.
Sambamba na kuwasili kwa Siku ya Quds Duniani; Mkutano wa Quds ambao ni turathi za pamoja za dini za mbinguni na mhimili wa umoja kati ya Umma wa Kiislamu ulifanyika nchini Tanzania kwa kuhudhuriwa na idadi kubwa ya vijana wapenda haki na wapenda uhuru kutoka vituo mbalimbali vya kielimu na vya kidini. Kulingana na IRNA,…
Waziri Mkuu Senegal akosoa uwepo wa kambi za kijeshi za Ufaransa nchini humo; asema huwenda zikafungwa
Waziri Mkuu wa Senegal, Ousmane Sonko, ameashiria uwezekano wa kufungwa kambi za kijeshi za Ufaransa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Amesema hayo katika hotuba yake mbele ya vyombo vya habari ambayo pia imegusia sarafu ya CFA inayoungwa mkono na Ulaya, mikataba ya mafuta na gesi na kile kinachotajwa kuwa haki za LGBTQ (mabaradhuli) zinazopigiwa…
Kenya na Uganda zaafikiana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta
Kenya na Uganda zimekubaliana kujenga kwa pamoja bomba la kusafirishia mafuta kutoka mjini Eldoret katika eneo la Bonde la Ufa nchini Kenya hadi Uganda. Baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba hilo, serikali ya Kampala itaweza kuagiza moja kwa moja bidhaa za mafuta yaliyosafishwa kupitia Nairobi. Rais William Ruto wa Kenya na mwenzake wa Uganda,…
Serikali ya Tanzania yatakiwa kubuni sheria maalumu ya ukatili dhidi ya wanawake
Serikali ya Tanzania imetakiwa kubuni sheria maalumu ya kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake. Watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania wameitaka serikali ya nchi hiyo kubuni sheria maalumu kwa ajili ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na wasichana kutokana na kuwepo kwa ongezeko la kubwa la ukatili katika kipindi cha hivi karibuni hali…
Tanzania, moja kati ya nguzo muhimu dhehebu la Shia Ithnashariya barani Afrika
Katika miongo 4 iliyopita, idadi ya Mashia nchini Tanzania imeongezeka, na Kituo cha Ahl al-Bayt ambayo ni moja kati ya madhehebu ya dini ya Kiislamu, kimepata nguvu nyingi. Asilimia kubwa ya wakazi wa Dar es Salaam, mojawapo ya miji ya kihistoria na muhimu nchini Tanzania na Afrika Mashariki, ni Waislamu kutoka kwenye dhehebu hili la…
Kampuni ya Ufaransa ya Total ilitangaza uanzilishi wa miradi iliyokumbwa na utata itakayopitia na kutumia sehemu ya ardhi iliyopo nchini Uganda na Tanzania
Kampuni ya mafuta na gesi ya Ufaransa ya TotalEnergies ilitangaza kuwa imeanza kutathmini ili kupata ardhi inayozunguka miradi yake yenye utata ya dola bilioni 10 nchini Uganda na Tanzania. Miradi hii inakosolewa na wanaharakati wa mazingira. Katika taarifa ya kampuni hii, imeelezwa kuwa “ujumbe huu utafanya tathmini ya taratibu zote zinazotekelezwa katika upatikanaji wa ardhi,…
Udanganyifu wa vyombo vya habari kwa utawala wa Kizayuni ili kuchochea hisia za Waafrika
Siku moja baada ya mashambulizi ya kimbunga cha Al-Aqsa, licha ya kwamba hakukua na jina la wafungwa wa Kitanzania waliochukuliwa na Hamas. Siku chache baada ya hapo ubalozi wa Tanzania nchini Israel ulitangaza kuwa kutokana na shambulio hilo la Hamas, ubalozi huo ulifuatilia hali za wanafunzi wa Kitanzania waliokuwa nchini Israel japo hawakuweza kupata taarifa…
El Nino barani Afrika; Mafuriko nchini Kenya na Tanzania yasababisha vifo vya watu 383
Mafuriko makubwa katika mataifa ya Afrika ikiwemo Kenya na Tanzania yamesababisha vifo vya takriban watu 383. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya ilitangaza kuwa takriban watu 228 waliuawa kutokana na mafuriko katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa gazeti la Rasha Today, mafuriko hayo pia yameathiri Hifadhi ya Kitaifa ya Safari…