Baraza la Usalama laidhinisha MONUSCO kuipa SADC msaada wa kilojistiki DRC
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepasisha azimio la kuidhinisha kikosi cha kusimamia amani cha umoja huo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO kutoa msaada wa kiutendaji na wa suhula na zana za kijeshi kwa ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) nchini DRC. Rasimu ya azimio hilo iliyowasilishwa na…
Tanzania yaunga mkono juhudi za amani za Uturuki, asema Rais Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisema kuwa nchi yake inaunga mkono juhudi za Uturuki za kutafuta suluhu na amani kwa mizozo ya kimataifa. “Vilevile tunaunga mkono wito wa dharura wa kusitishwa kwa mapigano kwa manufaa ya watu wa Gaza,” asema Hassan. “Pia tunaunga mkono wito wa dharura wa kusitishwa kwa mapigano kwa manufaa ya…
Serikali yatoa wito kwa Wakenya nchini Lebanon kuhama
Nchi kadhaa zimewataka raia wao kuondoka nchini Lebanon, huku hofu ikiongezeka ya mzozo mkubwa katika ukanda wa Mashariki ya Kati. Serikali ya Kenya kupitia Idara ya Mambo ya Nje ya Masuala ya Diaspora, imetoa wito kwa raia wake wanaoishi na kufanya kazi nchini Lebanon kujiandikisha ili kuhamishwa mara moja kutokana na hali ya mvutano inayoongezeka…
Tanzania inataka kuwafurusha Wamasai kwa ajili ya wanyamapori – Wenyeji wapinga Hatua hiyo
Wanajamii wanafanya kampeni kwa wafadhili wa kimataifa kufidia serikali yao na kukomesha ukiukaji wa haki. Dar-es-Salaam, Tanzania – Nadharia ya Joseph Oleshangay ni kwamba maafisa wa serikali katika nchi yake, Tanzania, wanaona watu kutoka jamii yake kuwa chini ya wanadamu. Mwanasheria huyo wa haki za binadamu mwenye umri wa miaka 36 na mwanachama wa kundi…
Shambulizi la kigaidi katika mji mkuu wa Somalia lasababisha vifo vya watu 30
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, takriban watu 30 waliuawa katika shambulizi la kigaidi usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu wa Somalia. Kwa mujibu wa ripoti ya IRNA ya Ijumaa usiku kutoka Shirika la Habari la Tas, walioshuhudia wameripoti ufyatuaji risasi na milipuko ya guruneti mjini Mogadishu. Pia, vyombo vya habari vya…
Tume ya uchaguzi nchini Uganda yatangaza tarehe ya uchaguzi mkuu wa 2026
Tume ya Uchaguzi ya Uganda (EC) imetangaza ramani ya uchaguzi iliyorekebishwa ikitangaza tarehe ya uchaguzi wa rais na wabunge wa 2026. Jaji Simon Byabakama, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi amesema uteuzi wa wagombea urais na ubunge utafanywa kati ya Septemba 17 na Oktoba 3, 2025. Byabakama alisema kampeni hizo zitaanza wiki ya pili ya Oktoba…
Rwanda na DRC zakubaliana kusitisha mapigano mashariki mwa Congo
Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano mashariki mwa DRC kuanzia Agosti 4 ya mwezi ujao katika mkutano uliofanyika mjini Luanda Angola. Hayo yametangazwa na ofisi ya rais wa Angola, nchi ambayo imekuwa mpatanishi katika duru kadhaa za mazungumzo ya kumaliza uhasama kati ya…
Baraza Kuu la Waislamu Kenya launga mkono mazungumzo ya kitaifa
Baraza Kuu la Waislamu Nchini Kenya (SUPKEM) limeunga mkono mazungumzo kuhusu masuala ambayo yameibuliwa vijana wanaofanya maandamano dhidi ya serikakli ya Rais William Ruto maarufu kama na Gen Z ili kukomesha zogo la kisiasa linaloendelea kushuhudiwa nchini humo. Mwenyekiti wa Supkem, Hassan Ole Naado, amesema kuwa baraza hilo linataka muafaka wa kisiasa ufikiwe ili kuyashughulikia…