
Sonko, Nassir Kukutana Ana Kwa Ana Hafla Ya Azimio Tononoka
ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko, ameapa kuhudhuria mkutano wa hadhara unaotarajiwa kuongozwa na kinara wa ODM, Bw Raila Odinga, katika uwanja wa Tononoka ulio Mombasa kesho Jumamosi. Iwapo mkutano huo utafanyika ilivyopangwa, itakuwa ni mara ya kwanza Bw Sonko kukutana hadharani na Mbunge wa Mvita, Bw Abdulswamad Nassir, ambao wote ni wagombeaji ugavana…

Kina Mdee wasubiri hukumu
Baada ya kazi ya kuthibitisha barua za kukata rufaa kupinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya Chadema, wabunge hao wa viti maalumu sasa wameitwa ukumbini kusikiliza hukumu yao. Mchakato wa kuwahoji wabunge hao 19 wa viti maalumu ulianza rasmi katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam ambapo Baraza Kuu la Chadema linaendelea likiwa na…

Samia aeleza mkakati kupunguza makali ongezeko bei ya mafuta
Dar es Salaam; Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza mkakati wa kubana matumizi ya Serikali katika bajeti ya matumizi ili kupata fedha za kupunguza makali ya ongezeko la bei ya mafuta linalosababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa na huduma nchini. Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 9, 2022 katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari…

11 Wapigania nafasi ya kuwa Mgombea Mwenza Wa Raila
IDADI ya wanaosaka nafasi ya kuteuliwa mmoja wao awe mgombea mwenza wa Raila Odinga katika kinyang’anyiro cha urais sasa imepanda hadi 11. Hii ni baada ya kujumuishwa kwa Waziri wa Kilimo Peter Munya, Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya na mwenzake wa Nakuru Lee Kinyanjui katika orodha ya awali ya watu wanane. Kwenye taarifa aliyoitoa Jumamosi,…

Rais Suluhu Atangaza Siku Mbili Za Maombolezo Ya Kibaki
RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza siku mbili za maombolezo nchini humo kufuatia kifo cha Rais wa Tatu wa Kenya Mwai Kibaki. Maombolezo hayo ya kitaifa yanaanza leo Ijumaa Aprili 29 hadi Jumamosi 30, 2022. Kwenye taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Rais Alhamisi, Aprili 28, Rais Suluhu aliwaomba Watanzania waungane na Kenya kuomboleza Hayati…

Hatimaye Kibaki Azikwa Karibu Na Kaburi La Mama Lucy
RAIS wa tatu wa Jamhuri ya Kenya, Stanley Emilio Mwai Kibaki alizikwa Jumamosi nyumbani kwake Othaya, Nyeri. Mazishi ya Mzee Kibaki yalihudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta, naibu wake, William Ruto, kiongozi wa ODM, Raila Odinga ambaye alihudumu kama Waziri Mkuu katika serikali ya mseto iliyoongozwa na marehemu, makamu wake, Kalonzo Musyoka, miongoni mwa wanasiasa na…

Mmoja auawa na polisi nchini Nigeria katika maandamano ya Siku ya Al-Quds Duniani
Polisi wa Nigeria wamemuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa katika shambulizi lililofanywa dhidi ya waandamanaji wa Siku ya Al-Quds Duniani huko Zaria, Jimbo la Kaduna. Takriban mtu mmoja aliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati polisi walipowafyatulia risasi wanachama wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) wakati wa maandamano ya Siku ya Dunia ya Al-Quds…

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini asisitiza umuhimu wa uhusiano na Iran
Katika mazungumzo ya simu na Amir Abdullahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ameutaja uhusiano na Iran kuwa muhimu kwa nchi hiyo na kueleza matumaini yake kuwa, ziara inayokuja ya rais wa Iran mjini Pretoria italeta msukumo mkubwa katika uhusiano wa pande hizo mbili. Kwa mujibu wa Kundi la Sera za Kigeni la…