
Spika wa Bunge la Uganda, Jacob Oulanyah aaga dunia
Spika wa Bunge la Kitaifa la Uganda, Jacob L’Okori Oulanyah amefariki dunia akitibiwa nchini Marekani. Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametangaza kifo cha Oulanyah kupitia taarifa aliyoituma leo katika ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter inayosema kuwa: Wananchi wenzangu, nasikitika kutangaza kifo cha Mheshimiwa Jacob Oulanyah, Spika wa Bunge (la Uganda). Nilipokea habari…

Rais wa Algeria: Hatutasahau jinai za ukoloni wa Ufaransa
Rais wa Algeria amesema uhalifu wa Ufaransa nchini Algeria hautakabiliwa na nyakati za kisasa na kwamba kesi hiyo lazima ichunguzwe kwa haki na uwazi. Kwa mujibu wa Idhaa ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Fars, Rais wa Algeria, Abdel Majid Taboun alisisitiza siku ya Ijumaa, siku ya kumbukumbu ya uhuru wa nchi hiyo, kwamba…

Kenya yawawinda wanaoeneza chuki kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9
Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa ya Kenya (NCIC), inachunguza watu 51 kwa tuhuma za kusambaza matamshi ya chuki huku kaunti sita zikikihofiwa kukumbwa na vurugu za kisiasa katika kipindi hiki nyeti cha kampeni kali za kuwapigia debe wanasia wanaowania kiti cha rais wa nchi hiyo. Mwenyekiti wa NCIC, Samuel Kobia, amesema watu 36…

Umoja wa Mataifa: Udhalilishaji unaofanywa na serikali ya Sudan Kusini ni sawa na jinai za kivita
UN imesema kuwa viongozi na maafisa wa serikali ya Sudan Kusini wamekiuka haki za binadamu nchini humo; vitendo vilivyotajwa kuwa ni sawa na jinai za kivita. Ukiukaji huo wa haki za binadamu umewakumba pia watoto wa Sudan Kusini. Nchi hiyo changa zaidi duniani imekuwa ikishuhudia mapigano na ukosefu wa amani tangu ipate uhuru mwaka 2011;…

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameilaumu NATO kwa vita vya Russia nchini Ukraine
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameilaumu NATO kwa vita vya Ukraine na kusema kuwa atapinga wito wa kuilaani Russia. Matamshi haya ya Ramaphosa yanatia shaka iwapo atakubaliwa na Ukraine au nchi za Magharibi kama mpatanishi katika mzozo huo. Ramaphosa ambaye alikuwa akizungumza bungeni, amesema: “Vita hivyo vingeweza kuepukika kama NATO ingezingatia maonyo kutoka kwa viongozi…

Raila Odinga: Sitamwacha Uhuru Kenyatta iwapo nitashinda uchaguzi wa rais wa Agosti 9
Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, amesema kuwa hatamwacha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya iwapo atashinda uchaguzi wa Agosti 9, 2022. Raila amesema kuwa Rais Kenyatta amekuwa nguzo muhimu katika utulivu wa taifa na uchumi na kwamba yeyote atakayeshinda hastahili kumtelekeza. Amesema iwapo atashinda uchaguzi ujao ataendeleza uhusiano wake na Rais Uhuru Kenyatta na…

Moncef Marzouki amelaani kitendo cha jinai huku akiwaonya viongozi wa Saudia kwa kuua umati wa watu
Rais wa zamani wa Tunisia amewaonya viongozi wa Saudi Arabia kwa hatua yao ya kutekeleza adhabu ya kifo kwa watu 81 kwa siku moja na kuwaambia wajiandae kwa madhara ya hatua yao hiyo. Siku ya Jumamosi, wizara ya mambo ya ndani ya Saudia iitekeleza adhabu ya kifo kwa watu 81 ikidai kuwa watu hao wamefanya…

Mtoto wa Museveni hajajiuzulu, Jeshi la Uganda lakanusha
Jeshi la Uganda limesema leo Jumatatu kwamba mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye anatajwa kuwa ndiye atakayerithi miikoba ya baba yake kama rais ajaye wa Uganda, hajajiuzulu. Muhoozi Kainerugaba alitangaza kwenye mtandao wa Twitter mnamo Machi 8 kwamba amestaafu kutoka kwenye jeshi baada ya utumishi wa zaidi ya miaka 20….