AFRIKA

Shambulio la kigaidi magharibi mwa Nigeria, 14 wauawa huku 15 wakitekwanyara

Shambulio la kigaidi magharibi mwa Nigeria, 14 wauawa huku 15 wakitekwanyara

Magaidi wenye silaha wamevishambulia vijiji viwili katika jimbo la Niger magharibi mwa Nigeria na kuua watu 14 na kuwateka nyara wengine 15. Gazeti la Tribune la nchini Nigeria limeripoti kuwa, magaidi waliokuwa na silaha jana Jumatatu waliwafyatulia risasi na kuwaua wakazi 14 wa vijiji hivyo viwili katika jimbo la Niger magharibi mwa nchi hiyo sambamba…

Kenya miongoni mwa nchi zitakazoanza kutengeneza chanjo za Covid-19 kwa teknolojia ya mNRA

Kenya miongoni mwa nchi zitakazoanza kutengeneza chanjo za Covid-19 kwa teknolojia ya mNRA

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, nchi sita za Afrika zimechaguliwa kuanza utengenezaji wao wa chanjo za Covid-19 kwa kutumia teknolojia ya mfumo wa mRNA. Kenya, Afrika Kusini, Nigeria, Senegal, Misri na Tunisia zimechaguliwa kuwa nchi za kwanza kupokea teknolojia ya mRNA kutoka kituo Shirika la Afya Duniani (WHO) cha kimataifa, katika bara hilo…

Mali imeitaka Ufaransa kuwaondoa askari wake walioko nchini haraka iwezekanavyo

Mali imeitaka Ufaransa kuwaondoa askari wake walioko nchini haraka iwezekanavyo

Serikali ya mpito ya Mali imeitaka Ufaransa kuwaondoa bila kuchelewa askari wake wa operesheni Barkhane na Takuba nchini Mali. Takwa hilo la Mali linakuja masaa machache tu baada ya tangazo la Rais Emmanuel Macron na washirika wake la kuwaondoa askari wa nchi zao kutoka Mali katika miezi michache ijayo. Akitangaza uamuzi huo kupitia televisheni ya…

Nigeria ; Waislamu waandamana kulaani mauaji ya kimbari nchini Yemen na jinai za muungano vamizi uliopo chini ya uongozi wa Saudi Arabia

Nigeria ; Waislamu waandamana kulaani mauaji ya kimbari nchini Yemen na jinai za muungano vamizi uliopo chini ya uongozi wa Saudi Arabia

Katika kuitikia wito wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Waislamu nchini Nigeria wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja, kulaani jinai za muungano vamizi unaoongozwa na utawala wa Saudi Arabia ambao umeendelea kutenda jinai na mauaji ya kimbari nchini Yemen. Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu yenye jumbe mbalimbali wametangaza himaya na uungaji…

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini: Hivi karibuni tutachukua hatua dhidi ya ubaguzi wa rangi wa Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini: Hivi karibuni tutachukua hatua dhidi ya ubaguzi wa rangi wa Israel

Faraan : Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini alikosoa vikali utawala huo ghasibu na ubaguzi wake wa rangi dhidi ya Wapalestina. Kulingana na Fars News Agency International Group; Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Nalidi Bandur katika hotuba yake mbele ya bunge aliukosoa utawala wa Kizayuni wa Israel kwa uvamizi wake…

Rais Abdelmadjid Tebboune : Morocco na Israel chanzo cha fitina nchini Algeria

Rais Abdelmadjid Tebboune : Morocco na Israel chanzo cha fitina nchini Algeria

Faraan : Rais wa Algeria amesema kuwa Israel na Morocco zinafanya njama ya kuibua hitilafu kati ya Ofisi ya Rais na Jeshi la Algeria na kuzusha fitna nchini humo. Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria amesema kwamba, Morocco na utawala wa Kizayuni wa Isarael ndio wanaoendesha njama za kuzusha fitina na kueneza…

Mlipuko uliotikisa Mogadishu / Mji Mkuu wa Somalia

Mlipuko uliotikisa Mogadishu / Mji Mkuu wa Somalia

Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada katika mkutano wa hadhara uliokua katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, huku wanamgambo wa al-Shabaab wakishambulia vituo vya polisi. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, waziri wa usalama wa mambo ya ndani wa Somalia alisema kuwa mnamo Jumatano asubuhi, wanamgambo wa al-Shabaab walishambulia vituo vya polisi na…

Vituo vya polisi Mogadishu vyashambuliwa na Al Shabaab

Vituo vya polisi Mogadishu vyashambuliwa na Al Shabaab

Wanamgambo wa kundi la al Shabaab wa nchini Somalia mapema leo wameshambulia vituo vya polisi na vya upekuzi katika mji mkuu Mogadishu. Kundi hilo la kigaidi limefanya hujuma hiyo huku Somalia ikijiandaa kwa uchaguzi wa rais ulioakhirishwa mara kadhaa. Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, watu sita wamepoteza maisha katika mashambulizi ya leo ya al Shabaab…