
UTATA MASHARIKI YA KATI: Tahadhari yatolewa kwa Tanzania mgogoro wa Marekani, Iran
Mzozo huo umetokana na mpango wa nchi ya Iran wa kuzalisha nyuklia ikisema ni kwa ajili ya umeme, huku Marekani ikidai kuwa nchi hiyo ina mpango wa siri wa kutengeneza silaha za nyuklia. Kutokana na hofu hiyo, nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na China zilikubaliana kuiwekea vikwazo Iran iwapo itaendelea na mpango huo.Mwaka 2015…

Je, Wachaga wana asili ya Uyahudi?
Wakati fulani Wachaga walinasibishwa na Uyahudi. Ilidaiwa kuwa kabila hilo lina nasaba na Wayahudi wa Ethiopia. Hata hivyo, kabila hilo linalopatikana kaskazini mwa Tanzania, linaelezwa kuwa limetokana na mchanganyiko wa wahamaji kutoka makabila mbalimmbali wakiwamo Wakamba, Wataita, Wamasai na Wasambaa. Miongoni mwa waliofanya utafiti na kuandika kuhusu hili ni aliyekuwa mhadhiri wa historia katika Chuo…

Tanzania yatangaza miradi ya kimkakati maonyesho Dubai
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dotto James amesema Tanzania inatangaza miradi mikubwa ya kimkakati katika maonyesho ya kimataifa yanayofanyika Dubai katika Falme za Kiarabu (UAE). James ameyasema hayo leo Jumanne Oktoba 26 jijini Dar es Salaam wakati akitoa mrejesho wa ziara yake huko Dubai ambako alikwenda kuangalia ushiriki wa Tanzania…

Waziri Mkuu wa Sudan kutangaza kujiuzulu katika masaa machache yajayo
Duru za karibu na Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok zimetangaza kwamba waziri mkuu huyo atatangaza kujiuzulu katika kipindi cha masaa machache yajayo. Faraan: Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti habari hiyo na kuzinukuu duru mbili zilizoko karibu na Hamdok zikisema kuwa, waziri mkuu huyo wa Sudan atatangaza kujizulu masaa machache yajayo. Hamdok alirejea madarakani tarehe…

Ghana yawapiga marufuku wasafiri wa utawala wa Kizyauni kutokana na omicron
Serikali ya Ghana imepiga marufuku kuingia nchini humo wasafiri wote wanaotoka katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel, kama njia ya kupambana na maambukizo ya kirusi kipya cha corona kiitwacho omicron. Faraan: Mtandao wa habari wa “Ghana Web” umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, amri hiyo imeanza kutekelezwa…

Maelfu waandamana Sudan kupinga utawala wa kijeshi
Maelfu ya raia wa Sudan Jumapili wameshiriki katika maandamano makubwa katika mji mkuu Khartoum na miji mingine kote nchini humo kupinga mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba 25. Faraan: Waandamanaji hao pia wamepinga mkataba wa hivi karibuni uliomrejesha madarakani waziri mkuu wa kiraia Abdalla Hamdok. Maandamano hayo ya Jumapili ni ya kuadhimisha mwaka wa tatu wa…

Vikwazo vya Marekani vinaweza kuwa Rahisi, lakini si vya bei nafuu
Mwaka wa 2021 unapokaribia kuisha, jumuiya ya kimataifa inakabiliwa na majanga kadhaa ya kibinadamu na yale ya usalama yanayoibuka kila uchao, hata zaidi ya janga la kimataifa ambalo limeikumba dunia kwa miaka miwili. Ethiopia inakumbwa na vita tata vya ndani ya nchi baina yao wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimesababisha maafa ya kiasi kikubwa ya kibinadamu,…

Ethiopia: Baraza la Haki za Binadamu la UN linatumika kisiasa
Ethiopia imekosoa kufanyika kwa kikao maalumu cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kujadili na kutathmini visa vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo kufuatia mzozo unaoendelea kati ya serikali na waasi wa Tigray. Faraan: Balozi wa Ethiopia katika Umoja wa Mataifa Zenebe Kebede amelishutumu baraza hilo akisema limetekwa na fikra…