
Watu 28 wauawa katika mashambulizi ya jeshi la Ethiopia
Vyombo vya habari vimewanukuu wanamgambo wa kundi la Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray wakisema kuwa mashambulizi ya anga ya ndege za jeshi la Ethiopia yameua watu 28 na kujeruhi wengine 76 katika mji mmoja wa kaskazini mwa nchi hiyo. Faraan: Msemaji wa Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) amesema kuwa, watu…
Magaidi 100 wa Al Qaida wauawa katika mpaka wa Burkina Faso na Mali
Mamluki 100 wenye mfungamano na kundi la kigaidi la al Qaida wameuawa katika oparesheni za pamoja kati ya Burkina Faso na Niger katika mpaka wa nchi mbili hizo. Faraan: Jeshi la Burkina Faso jana usiku lilitangaza kuwa magaidi hao waliuawa katika oparesheni za pamoja ya nchi mbili hizo kuanzia Novemba 25 hadi tarehe 9 mwezi…

Amnesty International: Ghasia kubwa za Sudan Kusini zinaweza kuwa uhalifu wa kivita
Ripoti iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International imesema kuwa kuongezeka kwa mapigano kati ya makundi hasimu yenye silaha yanayoshirikiana na serikali na vikosi vya upinzani nchini Sudan Kusini mwaka huu kumeua makumi ya raia na kuibua “vurugu zisizotasawarika” ambazo zinaweza kuwa uhalifu wa kivita. Faraan: Katika ripoti yake mpya iliyotolewa…

Idadi ya waliouawa katika machafuko ya Darfur, Sudan yafikia 88
Idadi ya watu waliouawa katika ghasia na machafuko yaliyotokea baina ya makabila hasimu katika jimbo la Darfur huko magharibi mwa Sudan imeongezeka na kufikia 88 huku wengine 84 wakijeruhiwa. Faraan: Kabla ya hapo iliripotiwa kuwa, watu 50 wameuawa katika ghasia na machafuko yaliyotokea baina ya makabila hasimu katika jimbo la Darfur huko magharibi mwa Sudan….

Wafungwa 21 waliotoroka baada ya kushambulia jela moja nchini Nigeria, wakamatwa
Maafisa wa Nigeria wamethibitisha taarifa zinazosema kuwa, wafungwa 21 kati ya waliotoroka baada ya jela moja kushambuliwa na watu wenye silaha katika jimbo la Plateau la katikati mwa nchi hiyo, wamekamatwa na kurejeshwa jela. Faraan: Kwa uchache watu 11 waliuwa na wafungwa 252 walitoroka baada ya watu wenye silaha kuivamia jela hiyo iliyoko katika mji…

Maandamano ya kupinga safari ya waziri wa vita wa Israel yashamiri nchini Morocco
Maandamano ya kupinga safari ya waziri wa vita wa Israel nchini Morocco yamesambaa zaidi katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Faraan: Wananchi wa Morocco katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ukiwemo mji mkuu, Rabat, wamefanya maandamano wakipinga safari ilioyofanywa nchini humo na waziri wa vita wa utawala haramu wa Israel, Benny…

Rais wa Algeria: Nchi za Kiarabu zinapaswa kulisaidia taifa la Palestina dhidi ya utawala haramu wa Israel
Rais wa Algeria amesisitiza udharura wa nchi za Kiarabu kushirikiana kwa ajili ya kusaidia mapambano ya ukombozi ya wananchi wa Palestina dhidi ya utawala vamizi na ghasibu wa Israel. Faraan: Abdelmadjid Tebboune ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas aliyeko safari nchini Algeria ambako ametangaza msaada wa…

Jeshi la serikali ya Ethiopia lakomboa miji 3 ya kimkakati katika mapigano na waasi wa Tigray
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed asema kwamba vikosi vya nchi yake vimedhibiti tena udhibiti miji 3 ya kimkakati katika eneo la kaskazini la Amhara iliyokuwa mikononi mwa kundi la Tigray People’s Liberation Front. Faraan: Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema kuwa vikosi vya serikali vimefanikiwa kuteka tena miji ya kimkakati ya Disi, Kombolcha na Bati…