Jinsi Mzozo wa Israel na Hamas unavyoathiri nchi za Afrika
Mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas sio tu kwamba umesababisha maafa ya kibinadamu lakini pia umesababisha tishio linaloweza kuathiri utulivu na ustawi wa uchumi wa dunia. Huku mzozo huo ukiongezeka, nchi za Afrika zinaweza kukabiliana na changamoto na fursa mbalimbali kuhusu biashara, nishati, usalama na diplomasia. Biashara Mojawapo ya athari kuu za mzozo huo…
Judith Suminwa Tuluka ateuliwa kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini Kongo DR
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amemteua waziri wa mipango Judith Suminwa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo. Suminwa ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo wa uwaziri mkuu nchini Kongo DR. Uteuzi wa Suminwa unakamilisha wiki kadhaa zilizogubikwa na hali ya sutafahamu kuhusu wadhifa huo. Katika hotuba aliyotoa kupitia televisheni ya taifa,…
Maandamano 100 yafanyika katika miji 52 nchini Moroko katika kuunga mkono Palestina
Mamia ya wananchi wa Moroko walifanya maandamano katika miji mbalimbali ya nchi hii wakiwaunga mkono wananchi wa Palestina na kulaani vitendo vya Israel. Gazeti la “Al-Arabi Al-Jadeed” limeripoti kuwa maandamano 100 ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina yamefanyika katika miji 52 ya Maghreb, na washiriki wa maandamano hayo walipiga nara dhidi ya Israel. Kwa mujibu…
Watu 18 wapoteza maisha, maelfu wapoteza makazi baada ya kimbunga Madagascar
Kimbunga cha kitropiki kilichoikumba Madagascar kimesababisha vifo vya watu wasiopungua 18 na wengine kadhaa kutoweka baada ya kupiga eneo la kaskazini mwa kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi mapema wiki hii. Taarifa za hivi punde zimebaini kuwa kimbunga hicho kimesababisha mafuriko makubwa, na kuwacha takriban watu 47,000 wakilazimika kuhama makao yao. Aidha kimbunga hicho kimsababisha…
Rais Museveni amteua mwanawe kuwa Mkuu wa Majeshi ya Uganda
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemteua mwanawe wa kiume, Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Wizara ya Ulinzi ya Uganda imetangaza habari hiyo leo Ijumaa bila kutoa maelezo ya kina. Taarifa ya wizara hiyo imesema Jenerali Kainerugaba amechukua nafasi ya Wilson Mbasu Mbadi, ambaye jana aliondolewa katika wadhifa…
Maafisa wa uchunguzi Afrika Kusini wapekua nyumba ya Spika anayetuhumiwa kupokea hongo
Maafisa wa Kitengo Maalumu cha Uchunguzi nchini Afrika Kusini wamepekua nyumba ya Spika wa Bunge kwa zaidi ya saa tano na kuchukua ushahidi kama sehemu ya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili kiongozi huyo za kupokea hongo alipokuwa waziri wa ulinzi. Kufanyika kwa operesheni hiyo ya msako na unasaji katika nyumba Bi Nosiviwe Mapisa-Nqakula, ambaye ni mbunge mkongwe katika…
Msisitizo wa afisa huyo wa zamani wa Mauritania juu ya umuhimu wa msaada wa kifedha kwa Gaza
Mkuu wa zamani wa Baraza la Fatwa la Mauritania alisema: “Hakuna kisingizio kinachokubalika kwa kupuuza misaada kwa raia wa Gaza.” Mohammad Al-Mukhtar Ould Mbaleh, akizungumza katika hafla ya ugawaji wa zawadi za mashindano makubwa ya kuhifadhi na kuhifadhi Qur’ani yaliyoandaliwa na Redio Mauritania, alibainisha kuwa kutokana na matukio ya sasa ya Gaza, upinzani (dhidi ya…
Taharuki yatanda Sudan Kusini baada ya watu 15 kuuawa Pibor
Hali ya wasi wasi imetanda nchini Sudan Kusini kufuatia mauaji ya watu 15 yaliyotokea katika eneo la Pibor, mashariki mwa nchi hiyo. Abraham Kelang, Waziri wa Habari wa Eneo Pana la Pibor aliliambia shirika la habari la Reuters jana Jumatano kuwa, miongoni mwa waliouawa katika shambulizi hilo la wabeba silaha ni Kamishna wa Kaunti ya…