Utawala wa Kizayuni waondolewa kabisa katika ngazi ya usimamizi na Umoja wa Afrika
Mnamo Februari 2023, wakati wa mkutano wa awali wa Umoja wa Afrika, wajumbe wa Israeli walifukuzwa kutoka kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Afrika. Afrika Kusini na Algeria, ndio nchi mbili zilizokuwa nyuma katika kuwatenga wawakilishi wa Kizayuni, nakupinga kuwepo kwa utawala wa Kizayuni kuwa mwanachama mwangalizi katika Umoja wa Afrika. Kulingana na Le Monde,…
Israel iliomba kukataliwa kwa malalamiko mapya ya Afrika Kusini katika Mahakama ya The Hague
Tel Aviv iliiomba Mahakama ya Hague kukataa ombi jipya la #Afrika_Kusini la kutoa amri ya dharura kuhusu operesheni ya jeshi la #Israeli huko #Rafah. Katika nyaraka zilizochapishwa hivi majuzi na Mahakama ya Kimataifa ya Haki, Israel imesema kuwa hukumu ya awali iliyotolewa na mahakama hii inajumuisha “hali ya jumla ya uhasama huko Gaza” na kwa…
Ripoti ya kulengwa kwa meli iliyopo kaskazini mwa Djibouti
Vyanzo vya habari vya Uingereza vilisema kwamba meli ya kibiashara ililengwa na ndege isiyo na rubani katika maji katika masafa ya kilomita 110 kaskazini mwa Djibouti. Siku ya Jumanne asubuhi, vyanzo vya ndani viliripoti tukio la usalama kwa meli katika eneo la mlango bahari la “Bab Al-Mandab”. Shirika la Usafiri wa Majini la Uingereza limesema…
Mashambulizi makubwa ya mabomu ya Rafah wakati huo huo mazungumzo ya Cairo yakiendelea
Jeshi linalokalia kwa mabavu la Israel liliharibu kabisa msikiti na nyumba zilizokua katika maeneo hayo kwa kuongeza mashambulizi ya anga na mizinga katika mji wa Rafah. Mji wa Rafah, ambao ni kimbilio la mwisho la wakimbizi milioni 1.7 wa Gaza, uko chini ya mashambulizi makali zaidi ya anga na mizinga katika muda wa saa 24…
Makamu wa Rais wa Zimbabwe asema, serikali itazuia ufadhili wa masomo kwa LGBTQ+
Makamu wa Rais mwenye nguvu wa Zimbabwe amesema serikali itazuia ufadhili wa masomo wa chuo kikuu kwa vijana wanaojihusisha na maingiliano ya kingono ya watu wenye jinsia moja (LGBTQ+). Ufadhili wa masomo ya vyuo vikuu vya serikali kwa watu wa kati ya umri wa miaka 18 na 35 unafadhiliwa na GALZ, shirika la wanachama la…
Umoja wa Afrika: Jumuiya ya kimataifa haipaswi kufumbia macho jinai dhidi ya Palestina
Katika hotuba yake hii leo, mkuu wa Umoja wa Afrika ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuzingatia ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza. Ghazali Osmani, Mkuu wa Umoja wa Afrika amesema kuhusiana na suala hilo: Jumuiya ya kimataifa haiwezi kufumbia macho ukandamizaji unaotokea Palestina. Mkuu wa…
Congo DR yaiomba jamii ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda ili iache ‘kuwaunga mkono waasi wa M23’
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeiomba jamii ya kimataifa kuiwekea vikwazo nchi jirani ya Rwanda ikiituhumu kuwasaidia waasi wa M23 mashariki mwa nchi hiyo. Akizungumza na vyombo vya habari, msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Patrick Muyaya, amesema kuwa kamwe hatajadiliana na kundi la M23, ingawa kundi hilo limesisitiza kuwa liko tayari…
Umoja wa Afrika wazuia ujumbe wa Israel kuingia katika makao yake makuu
Chanzo cha kidiplomasia cha Afrika kimeiambia televisheni ya Al Jazeera ya Qatar kwamba Umoja wa Afrika umewazuia wajumbe wa utawala ghasibu wa Israel kuingia katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, ambao walikuwa wameomba kukutana na maafisa wa Afrika kwa madhumuni ya kuwasilisha maoni ya serikali ya Tel Aviv kuhusu vita vinavyoendelea huko…