AFRIKA

Wanawake nchini Kenya wafanya sherehe ya giza katika siku ya wapendanao

Wanawake nchini Kenya wafanya sherehe ya giza katika siku ya wapendanao

Mamia ya wanawake wa Kenya wafanya sherehe ya giza ya wapendanao kukomesha mauaji ya wanawake nchini. Huku watu ulimwenguni wakisherehekea Siku ya Wapendanao kwa maua na chokoleti, wanawake wa Kenya wakiwa katika maombolezo wakiwa wamevalia nguo nyeusi na kuwasha mishumaa na kushikilia waridi jekundu katika hafla ya kuwaenzi wanawake zaidi ya 30 waliouawa nchini humo…

Umoja wa Afrika wazuia ujumbe wa Israel kuingia katika makao yake makuu

Umoja wa Afrika wazuia ujumbe wa Israel kuingia katika makao yake makuu

Chanzo cha kidiplomasia cha Afrika kimeiambia televisheni ya Al Jazeera ya Qatar kwamba Umoja wa Afrika umewazuia wajumbe wa utawala ghasibu wa Israel kuingia katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, ambao walikuwa wameomba kukutana na maafisa wa Afrika kwa madhumuni ya kuwasilisha maoni ya serikali ya Tel Aviv kuhusu vita vinavyoendelea huko…

Jibu la Hizbollah la Lebanon kwa pendekezo la Ufaransa

Jibu la Hizbollah la Lebanon kwa pendekezo la Ufaransa

Ufaransa iliwasilisha pendekezo lake la maandishi kwa Beirut ili kumaliza mgogoro kati ya Hizbullah na utawala wa Kizayuni katika hatua tatu. Nchi hii pia imedai kurejeshwa kwa mazungumzo ya kuweka mipaka. Kulingana na Reuters, katika pendekezo hili, Ufaransa imezitaka pande zote mbili za mzozo kujiondoa kilomita 10 kutoka pande zote za mpaka. Mpango huu unaopendekezwa…

UHUSIANO WA ISRAELI-UGANDA WAKATI WA IDI AMIN

UHUSIANO WA ISRAELI-UGANDA WAKATI WA IDI AMIN

Katika muktadha wa uhusiano kati ya Israel na nchi za Kiafrika ulioanza kustawi mwishoni mwa miaka ya 1950, Uganda, iliyopata uhuru mnamo mwaka 1962, ina nafasi maalum. Israel ilijitolea juhudi na rasilimali nyingi katika kukuza uhusiano na nchi ya Uganda, na shughuli yake nchini Uganda katika miaka ya 1960 ilikuwa kati ya mapana zaidi barani…

Vita vya maneno kati ya Misri na Israel vinaendelea baada ya Tel Aviv kuihusisha Cairo na Oktoba 7

Vita vya maneno kati ya Misri na Israel vinaendelea baada ya Tel Aviv kuihusisha Cairo na Oktoba 7

Mvutano wa kidiplomasia kati ya Misri na utawala wa Kizayuni wa Israel umeongezeka kufuatia matamshi yenye utata yaliyotolewa na waziri wa Israel ya kuihusisha Cairo na matukio ya Oktoba 7. Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imetoa taarifa ya kulaani ilichokiita matamshi ya “kuaibisha” na “ya kutowajibika” ya waziri wa fedha wa mrengo wa…

Maandamano makubwa yafanyika Rabat kupinga uhusiano wa Morocco na Israel ‘mfanya mauaji ya kimbari’

Maandamano makubwa yafanyika Rabat kupinga uhusiano wa Morocco na Israel ‘mfanya mauaji ya kimbari’

Maelfu ya Wamorocco wamejitokeza tena kwenye barabara za mji mkuu wao Rabat kutoa wito wa kusitishwa uhusiano wa nchi yao na utawala wa Kizayuni wa Israel, ambao wameulaani na kuutaja kuwa kuwa ni mfanya “mauaji ya kimbari” katika Ukanda wa Gaza. Mwishoni mwa 2020, Morocco ilianzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel chini ya Mkataba wa Abraham…

Mzozo kati ya Israel na Palestina wasababisha mataifa ya Afrika kugawanyika

Mzozo kati ya Israel na Palestina wasababisha mataifa ya Afrika kugawanyika

Kenya, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo miongoni mwa nchi zinazounga mkono Israel – Misimamo ya nchi za Kiafrika kuhusu suala hili inategemea zaidi maslahi ya kisiasa na kijiografia (kulingana na uchambuzi). – Nchi kama Afrika Kusini na Algeria zimechukua msimamo mkali kwa ajili ya Wapalestina. Mzozo unaoendelea kati ya Israel na Hamas katika Ukanda…

Ufunguzi wa ubalozi wa 11 wa utawala wa Kizayuni barani Afrika

Ufunguzi wa ubalozi wa 11 wa utawala wa Kizayuni barani Afrika

Hapo jana utawala wa Kizayuni ulifungua ubalozi wake katika nchi ya Rwanda iliyoko Afrika Mashariki, na hivyo idadi ya balozi za utawala huo katika nchi za Afrika kufikia 11. Kwa mujibu wa Kituo cha Habari cha Palestina, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala wa Kizayuni, Yoval Rotim alifungua ubalozi…