The Intercept: Uhalifu wa kivita unaruhusiwa kwa Israel, ni haramu kwa Sudan
Makala iliyochapishwa kwenye tovuti ya habari ya Marekani, The Intercept, imekosoa misimamo ya kindumakuwili na ya kinafiki iliyochukuliwa na Marekani kuhusu mizozo ya kimataifa, ambayo ilidhihirika wazi katika kushughulikia uvamizi wa Israel kwenye Ukanda wa Gaza, na vita vinavyoendelea nchini Sudan kati ya jeshi rasmi na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF). Makala hiyo imesema…
Rais wa Senegal aakhirisha uchaguzi wa rais wa Februari 25 kwa muda usiojulikana
Rais Macky Sall wa Senegal ametangaza kuakhirisha kwa muda usiojulikana uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Februari 25, saa chache kabla ya kampeni rasmi kuanza. Katika hotuba yake kwa taifa siku ya Jumamosi, Sall alisema ametia saini amri ya kukomesha hatua ya awali iliyoweka tarehe hiyo, kwa sababu wabunge walikuwa wakiwachunguza majaji wawili wa Baraza la…
Rais wa Namibia afariki dunia akiwa na umri wa miaka 82
Rais wa Namibia Hage Geingob amefariki dunia mapema Jumapili ya leo ikiwa ni wiki kadhaa tu baada ya kugunduliwa kuwa na saratani. Ikulu ya Rais nchini Namibia imethibitisha habari ya kifo cha Rais wa nchi hiiyo na kueleza kuwa ni pigo kubwa kwa taifa hilo. Hage Geingob, aliyekuwa na umri wa miaka 82, ameongoza taifa…
Niger, Mali na Burkina Faso zajiondoa ECOWAS
Nchi tatu za Burkina Faso, Mali na Niger zilitangaza uamuzi wao wa kujiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) katika taarifa. Katika taarifa ya pamoja, viongozi wa Burkina Faso, Mali na Niger waliichukulia Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuwa shirika lililokabidhiwa kwa mataifa ya kigeni na kutangaza uamuzi wao…
Umoja wa Mataifa washtushwa na mauaji ya watu 50 nchini Mali
Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kusikitishwa na mauaji ya karibuni ya makumi ya watu nchini Mali. Katika taarifa jana Alkhamisi, Volker Turk amesema ameshtushwa na mauaji ya kiholela yaliofanywa na jeshi la Mali na askari ajinabi dhidi ya raia 25 katika kijiji cha Welingara katika eneo la Nara, katikati…
Ruto Alegeza Msimamo Kuhusu Vita vya Israel na Palestina Baada ya mazungumzo ya simu na Netanyahu
Rais William Ruto amelegeza msimamo wake kuhusu vita kati ya Israel na Palestina, ambavyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 27,000. Kupitia kwenye simu mnamo Alhamisi, Februari 1, Ruto alizungumza na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kuhusiana na vita katika Ukanda wa Gaza ambapo aliibua wasiwasi kuhusu mzozo wa kibinadamu. “Nimeelezea wasiwasi wa Kenya…
Kiongozi wa Mapinduzi ya Afrika: Wazayuni wanamalengo ya kuvunja uhusiano wa kihistoria kati ya Afrika na Palestina
Kiongozi wa mapinduzi dhidi ya Uzayuni wa Afrika amesema: Wazayuni wanataka kuvunja uhusiano wa kihistoria kati ya Waafrika, nchi za Kiarabu na Palestina. Kami Saba akiwa katika mkutano na waandishi wa habari juu ya mada ya mapambano ya Afrika dhidi ya ukoloni na upinzani wa Gaza dhidi ya adui wa kawaida, uliofanyika katika ukumbi wa…
ICC: Tunaamini pande zote mbili za vita nchini Sudan zimefanya uhalifu wa kivita Darfur
Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Karim Khan, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba kuna “sababu za kuamini” kwamba jeshi la Sudan, Vikosi vya Msaada wa Haraka, na vikundi washirika wao wamefanya uhalifu wa kivita huko Darfur. Karim Khan ameyasema hayo wakati akiwasilisha ripoti kuhusu ukiukaji wa sheria unaofanyika huko…