Waziri wa Afrika Kusini:’Mandela atakuwa anatabasamu’ kufuatia uamuzi wa ICJ dhidi ya Israel
Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini amesema kiongozi wa mapinduzi ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo Shujaa Nelson Mandela “atakuwa anatabasamu kwenye kaburi lake” kutokana na uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ambayo iliamuru utawala wa Kizayuni wa Israel kuchukua hatua zote zinazohitajika kuzuia vitendo vya mauaji ya kimbari huko Gaza. Ronald…
Karim Benzema amshitaki waziri wa Ufaransa kwa kumchafulia jina
Matamshi ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin yanayomhusisha Benzema na Muslim Brotherhood yameharibu sifa ya mwanasoka huyo maarufu, yanasema malalamiko. Karim Benzema amewasilisha malalamiko yake kuhusu kuchafuliwa jina na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Gerald Darmanin, ambaye mwaka jana alisema nyota huyo wa zamani wa Real Madrid alikuwa na…
Mizozo yaathiri mauzo ya bidhaa za Kenya nchini Tanzania na Uganda
Mizozo iliyoibuka baina ya Kenya na majirani zake kama Tanzania, Somalia, Uganda Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inatajwa kuwa na taathira hasi kwa biashara katika Ukanda wa Afrika Mashariki. Ripoti zinaonyesha kuwa, mauzo ya Kenya kwa nchi jirani za Uganda na Tanzania yamepungua tangu Oktoba mwaka jana huku kukiwa na uhusiano mbaya kati…
Kumbukumbu ya kifo cha shujaa na mpinzani wa ukoloni nchini Congo; Lumumba alikuwa nani na kwa nini aliuawa?
Ilichukua siku 200 pekee tangu Patrice Lumumba alipotoa hotuba yake ya kwanza ya kuunga mkono uhuru wa Kongo hadi alipouawa kupitia njama za serikali ya Ubelgiji. Kati ya Julai 30, 1960, Patrice Lumumba alipotoa hotuba yake ya kwanza ya epic kuunga mkono uhuru wa Kongo kutoka kwa ufalme wa kikoloni wa Ubelgiji, na Januari 17,…
Usafishaji wa kimbari nchini Sudan; Watu elfu 15 wauawa katika mji mmoja pekee
Umoja wa Mataifa, ukiwasilisha ripoti ya kushangaza, ulithibitisha vifo vya watu wapatao 15,000 wakati wa ghasia za Vikosi vya Msaada wa Haraka katika mji wa Sudan wakati wa miezi mitatu ya Aprili hadi Juni mwaka jana. “Vijana wa kiume walilengwa kwa risasi na Kikosi cha Msaada wa Haraka na, baada ya kuhojiwa, ikibainika kuwa wanatoka…
Kikao cha leo cha wakuu wa NAM Uganda; Iran yataka jumuiya hiyo itilie mkazo kuihami Palestina
Mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote NAM unafanyika leo katika mji mkuu wa Uganda, Kamapala huku Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikiwataka wanachama wa jumuiya hiyo kutilia mkazo uungaji mkono wao kwa taifa linalodhulumiwa la Palestina. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran,…
Maandamano ya kupinga utawala wa Kizayuni katika yapamba moto nchini Afrika Kusini
Maelfu ya watu kutoka Johannesburg nchini Afrika Kusini walipiga nara dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni wa Ghaza kwa kufanya maandamano makubwa siku ya Jumamosi. Maelfu ya wakaazi wa mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini walikusanyika mbele ya ubalozi mdogo wa Marekani katika mji huo Jumamosi na kutoa nara dhidi ya utawala wa Kizayuni….
Uganda ni mwenyeji kikao cha Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM)
Viongozi kutoka takriban mataifa 120 duniani wamekusanyika katika mji mkuu wa Uganda, Kampala kwa ajili ya Mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wanachama wa Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) ulioanza jana Jumatatu. Takriban wageni 4,000 kutoka mataifa mbalimbali wanachama walitarajiwa kuhudhuria mkutano wa kilele utakaoendelea kwa muda wa wiki…