Muslim Zanzibar yapata kituo chake cha kwanza kabisa cha Kiyahud
Mwaka uliopita, idadi ya wageni 400,000 walisafiri kwenda Zanzibar. Bila shaka miongoni mwao, wakiwa ni Wayahudi, ikiwa ni pamoja na maelfu ya Waisraeli. Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara zenye safari za moja kwa moja kutoka nchini Israel. vichochoro vyenye kupindapinda hupitia katika milango iliyochongwa kabla ya kumwagika…
Ripoti: Watu bilioni moja Afrika bado hawawezi kumudu lishe bora
Imebainika kuwa idadi kubwa ya watu barani Afrika – karibu asilimia 78, au zaidi ya watu bilioni moja – bado hawawezi kumudu lishe bora, ikilinganishwa na asilimia 42 katika kiwango cha kimataifa, na idadi inaongezeka. Haya yamo kwenye ripoti iliyozinduliwa Alhamisi huko Johannesburg, Afrika Kusini na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la chakula…
Fatma Karume: Muungano haujaathiri Wazanzibari
MJANE wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume, Fatma Karume amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haujawaathiri Wazanzibari. Alisema hayo nyumbani kwake Maisara visiwani Zanzibar wakati anazungumza na waandishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN). Fatma akasema tangu Tanganyika na Zanzibar ziungane mwaka 1964, hajaona kama muungano umewaathiri Wazanzibari kwa namna yoyote. Anasema…
Kodi mpya ya majengo haitazihusu nyumba zachini
MASHEHA wa Mkoa wa Mjini Magharibi, wameelezwa kuwa na wajibu wa kuwasimamia wamiliki wa majengo katika shehia zao kuhakikisha wanalipa kodi hiyo ili serikali iweze kupata fedha kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo. Mkuu wa wilaya ya Magharibi ‘B’ Hamida Mussa Khamis alieleza hayo wakati akifungua kikao kazi kwa masheha kwa wilaya tatu za Mkoa…
RAIS wa Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias Kuandikwa
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias Kuandikwa kwa uteuzi alioupata na kuahidi kuendelea kushirikiana nae. Rais Dk. Hussein Mwinyi aliyasema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa…
Mkimbizi wa zamani Abdullahi Mire mwenye asili ya Somalia atwaa tuzo ya UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR Jumanne limemtangaza Abdullahi Mire mkimbizi wa zamani na mwandishi wa habari ambaye amekuwa kinara wa kupigania haki ya elimu huku akikabidhi vitabu 100,000 mikononi mwa watoto wakimbizi nchini Kenya kuwa ndiye mshindi wa kimataifa wa tuzo ya wakimbizi ya Nansen mwaka huu 2023. Kamishna Mkuu UNHCR Filippo…
Watu 120 wafa kwa janga la mafuriko nchini Kenya
Idadi ya watu waliokufa kutokana na janga la mafuriko yaliyokumba maeneo kadhaa nchini Kenya imefikia 120. Ripoti zinasema kuwa, mbali na maafa hayo ya kiroho, maelfu ya makaazi yamesombwa na maji katika baadhi ya maeneo ya Kenya na kuwalazimisha watu kutafuta hifadhi. Takwimu hizo mpya zimetolewa na afisa wa ngazi ya juu wa wizara ya…
Maafa ya mafuriko yanaendelea Somalia, China yatoa msaada wa dola 140,000
Ubalozi wa China nchini Somalia umeseema kuwa nchi yake imetoa msaada wa takriban dola 140,000 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Somalia walioathiriwa na mafuriko yanayoendelea kusababisha maafa na ambayo hadi hivi sasa yameshepelekea zaidi ya watu milioni 1 na laki 7 kuyahama makazi yao katika pembe mbalimbali za nchi hiyo ya Pembe ya Afrika….